China yashinda medali ya kwanza ya dhahabu ya mchezo wa kupiga makasia kwenye bahari katika Michezo ya Olimpiki ya Vijana 2026

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2026

Su Juntao na Liu Lili (mbele) kutoka China wakishindana na Frida Wever Lozano na Enrique Cristiano Morelos Olivares wa Mexico katika raundi ya 16 bora ya mbio za kupiga makasia kwenye bahari kati ya timu za watu wawili wa jinsia mchanganyiko kwenye Michezo ya Olimpiki ya Vijana 2026 huko Saly, Senegal, Novemba 1, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Su Juntao na Liu Lili (mbele) kutoka China wakishindana na Frida Wever Lozano na Enrique Cristiano Morelos Olivares wa Mexico katika raundi ya 16 bora ya mbio za kupiga makasia kwenye bahari kati ya timu za watu wawili wa jinsia mchanganyiko kwenye Michezo ya Olimpiki ya Vijana 2026 huko Saly, Senegal, Novemba 1, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

SALY, Senegal - Su Juntao na Liu Lili wameshinda medali ya kwanza ya dhahabu ya China katika Michezo ya Olimpiki ya Vijana 2026 jana Jumatatu huko Saly, Senegal, wakitwaa taji la mbio za kupiga makasia kwenye bahari kati ya timu za watu wawili wa jinsia mchanganyiko, wakati mchezo huo wa kupiga makasia kwenye bahari ukionekana kwa mara kwanza katika Michezo hiyo ya Olimpiki.

Wawili hao walitumia muda wa dakika 2 na sekunde 22.37 katika eneo la sehemu moja ya magharibi ya Ufukwe wa Saly, wakimaliza mbio hizo sekunde 6.58 mbele ya Lukas Schoenhuber na Alena Lux wa Austria. Raphael de Boussac na Elisa Guilloton wa Ufaransa wameshinda medali ya shaba.

Ushindi huo unawafanya Su na Liu kuwa mabingwa wa kwanza wa Olimpiki ya Vijana katika mbio za kupiga makasia kwenye bahari kati ya timu za watu wawili wa jinsia mchanganyiko, baada ya kutwaa taji lao la vijana chini ya umri wa miaka 19 (U19) waliloshinda kwenye Fainali za Dunia za Kupiga Makasia Kwenye Bahari huko Qingdao, China, mwezi uliopita.

"Nilihisi wasiwasi kwa kweli. Hatukupata muda wa kupumzika baada ya mashindano ya dunia, hivyo inachosha sana," amesema Liu.

"Sote wawili ni wenye nguvu zaidi, hivyo hii ndiyo sifa yetu bora; na tulijitahidi kadiri tuwezavyo kwenye bahari," ameongeza Su.

Kocha wa China, Fei Penghui, amesema wawili hao waliingia kwenye mashindano hayo wakiwa washindani wenye nguvu ya kushiriki mashindano baada ya kupata mafanikio yao kwenye mashindano huko Qingdao.

Fei pia amesisitiza umuhimu wa kushinda medali hiyo ya dhahabu katika mchezo ambao unaonekana kwa mara yake ya kwanza katika Michezo ya Olimpiki ya Vijana.

"Michezo ya Olimpiki ya Vijana ni fursa ya kipekee maishani. Wamepata nafasi zao hapa kupitia kufanya juhudi kubwa," amesema.

Su na Liu (mbele) wakishindana dhidi ya Lozano na Morelos Olivares katika hatua ya 16 bora ya mbio za kupiga makasia kwenye bahari kati ya timu za watu wawili wa jinsia mchanganyiko. (Xinhua/Chen Wei)

Su na Liu (mbele) wakishindana dhidi ya Lozano na Morelos Olivares katika hatua ya 16 bora ya mbio za kupiga makasia kwenye bahari kati ya timu za watu wawili wa jinsia mchanganyiko. (Xinhua/Chen Wei)

Kocha mkuu wa China, Muitaliano Francesco Cattaneo, amewasifu wawili hao kwa kudumisha kiwango chao kizuri baada ya ushindi wao wa taji la dunia hivi karibuni.

"Baada ya kushinda medali ya dhahabu huko Qingdao, wameonesha tena kiwango chao cha juu katika Michezo ya Olimpiki ya Vijana," amesema Cattaneo. "Kurudia mafanikio ya namna hiyo ni jambo gumu sana, na wamefanya vizuri sana."

Mbio hizo za kupiga makasia kwenye bahari zinahusisha kufanya mbio kwenye mchanga na kupiga makasia kwenye eneo moja pana la maji, kabla ya mbio za mwisho kuelekea mstari wa kumalizia. Mchezo huu pia utaonekana kwa mara ya kwanza kwenye Michezo ya Olimpiki ya timu za watu wazima jijini Los Angeles mwaka 2028.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha