Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Intaneti Duniani Wafunguliwa, kutarajia kwa Pamoja AI inayonufaisha watu wote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2026

Picha hii ilipigwa tarehe 3 Novemba 2026, ikionyesha hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Intaneti Duniani (WIC) 2026. (Xinhua/Zhang Yuwei)

Picha hii ilipigwa tarehe 3 Novemba 2026, ikionyesha hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Intaneti Duniani (WIC) 2026. (Xinhua/Zhang Yuwei)

Katika Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Intaneti Duniani (WIC) 2026 uliofunguliwa Jumanne, teknolojia ya chanzo huria, ilifuatiliwa zaidi kwenye mjadala, na washiriki walitoa wito wa kufanya ufunguaji mlango na ushirikiano katika nyanja ya AI na kunufaika pamoja na matokeo ya uvumbuzi kwenye mtandao wa Intaneti.

Mkutano huu wa kilele ulifanyika huko Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, na wajumbe 1,800 hivi kutoka nchi na maeneo 138 wamehudhuria kwenye mkutano huo. Mkutano ulifanyika chini ya Kaulimbiu ya “Kujenga Pamoja Mustakabali wa Kidijitali na AI ulio wa Ufunguaji Mlango na Ushirikiano, wa Usalama na wa Manufaa kwa Wote — Kushirikiana Kujenga Jumuiya ya Mtandao wa Intaneti Yenye Mustakabali wa Pamoja."

Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, alitoa hotuba kwenye hafla ya ufunguzi ya mkutano huo wa kilele, akitoa wito wa kutaka pande zote kufanya juhudi za kujenga jumuiya ya mtandao wa Intaneti yenye mustakabali wa pamoja.

Li Qiang alisema: "China itaendelea kufanya uvumbuzi unaofungua mlango, kuhimiza uhamishaji wa teknolojia na ujuzi kunufaisha wote, na kushirikiana na pande zote katika kujenga mfumo wa ikolojia wa uvumbuzi wa kidijitali wa dunia nzima ulio wa ufunguaji mlango, jumuishi, na unaojaa nguvu hai."

Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Hispania ambaye pia ni Waziri wa Wafanyakazi na Uchumi wa Kijamii wa nchi hiyo, Yolanda Diaz Perez, alipotoa hotuba kwenye hafla ya mkutano, alisema kuwa mkutano wa kilele wa Wuzhen "umeonyesha njia ya kufanya usimamizi kwa pamoja", na "teknolojia ya AI inapaswa kuwahudumia binadamu na kuwaletea ustawi".

"Tunataka AI ya chanzo huria na ya jumuishi," alisema. "Kila mtu anapaswa kupata manufaa kutoka kwa teknolojia ya AI."

Mkutano wa Kilele wa Wuzhen ulifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2014, ambapo maofisa wa serikali, wajumbe wa mashirika ya kimataifa, wakuu wa kampuni za teknolojia na watafiti wanakufanyika pamoja na kujadili maendeleo na usimamizi wa mtandao wa Intaneti.

Maonyesho ya “Mwanga wa Intaneti” ya Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 pia yalifunguliwa Jumatatu huko Wuzhen, yakilenga kuonyesha mafanikio ya maendeleo ya mtandao wa Intaneti wa AI.

Tarehe 2 Novemba 2026, katika Maonyesho ya “Mwanga wa Intaneti” ya Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 (2026 WIC) yaliyofanyika Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang, mfanyakazi mmoja anaonyesha jinsi ya kucheza piano kwa mkono wa bandia. (Xinhua/Liu Yun)

Tarehe 2 Novemba 2026, katika Maonyesho ya “Mwanga wa Intaneti” ya Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 (2026 WIC) yaliyofanyika Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang, mfanyakazi mmoja anaonyesha jinsi ya kucheza piano kwa mkono bandia. (Xinhua/Liu Yun)

Tarehe 2 Novemba 2026, mtembelezi mmoja akitazama zana na vifaa vya AI vya ulinzi wa usalama katika Maonyesho ya “Mwanga wa Intaneti” ya Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 (2026 WIC) yaliyofanyika Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang. (Xinhua/Liu Yun)

Tarehe 2 Novemba 2026, katika Maonyesho ya “Mwanga wa Intaneti” ya Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 (2026 WIC) yaliyofanyika Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang, roboti ya AI ikionyesha ufundi wa kufanya uchukuzi viwandani. (Xinhua/Liu Yun)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha