Kampuni 500 zenye nguvu kubwa zaidi duniani na zinazoongoza sekta zao zashiriki kwa wingi zaidi Maonyesho ya Uagizaji wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2026

Uwanja wa kusini wa Kituo cha Kitaifa cha Mikutano na Maonyesho (Shanghai) umepambwa upya kwa ajili ya kukaribisha siku ya kufunguliwa kwa Maonyesho ya Tisa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (picha ilipigwa tarehe 26 Oktoba). (Xinhua/Fang Zhe)

Uwanja wa kusini wa Kituo cha Kitaifa cha Mikutano na Maonyesho (Shanghai) umepambwa upya kwa ajili ya kukaribisha siku ya kufunguliwa kwa Maonyesho ya Tisa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (picha ilipigwa tarehe 26 Oktoba). (Xinhua/Fang Zhe)

Maonyesho ya Tisa ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa wa China (CIIE), yatakayofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 10 mwezi huu, yamevutia zaidi ya kampuni 300 zilizopo kwenye orodha ya Fortune ya kampuni 500 zenye nguvu kubwa zaidi duniani, na zile zinazoongoza katika sekta zao kushiriki kwenye maonesho hayo, hali ambayo imeweka rekodi mpya tangu maonyesho hayo yaanzishwe, na mvuto wa soko kubwa la China unaonekana mwaka hadi mwaka.

Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa wa China ni maonyesho ya kwanza ya kitaifa duniani ya mada ya uagizaji wa bidhaa. Maonesho hayo ya mwaka huu yatahusisha washiriki wa nchi, maeneo na mashirika ya kimataifa 162, na kampuni washiriki kutoka nchi mbalimbali watafikia zaidi ya 4,100.

Kampuni zitakazoshiriki kwenye maonesho hayo kwa mara ya kwanza zitafikia zaidi ya 2,000 mwaka huu, zikiwemo pamoja na chapa ya mitindo ya Marekani Ralph Lauren, Kundi la dawa la Pierre Fabre la Ufaransa, kampuni ya chokoleti ya Godiva ya Ubelgiji, na kampuni nyingine zilizopo kwenye nafasi za 500 zenye nguvu kubwa zaidi duniani, na zile zinazoongoza katika sekta zao.

Bidhaa zenye uwakilishi ambazo zinatolewa kwa mara ya kwanza duniani, zinazoonyeshwa kwa mara ya kwanza barani Asia, na zinazoonyeshwa kwa mara ya kwanza nchini China zinatazamiwa kufikia rekodi mpya ya juu katika maonyesho hayo ya mwaka huu.

Maonyesho hayo ya CIIE yanayofanyika kila mwaka na kufanyika vizuri zaidi mwaka hadi mwaka yanatoa ishara muhimu: China siku zote inashikilia ahadi yake ya kufungua mlango kwa uwekezaji wa kimataifa na biashara ya kimataifa.

Katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, uagizaji wa bidhaa nchini China ulifikia Yuan trilioni 16.74 (takriban dola za kimarekani trilioni 2.51), ambazo ni ongezeko la asilimia 22.3 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kasi ya ongezeko imefikia pointi 5.9 za asilimia kuliko uuzaji wa bidhaa nje.

Tokea mwaka 2018, maonyesho hayo yamefanyika kwa mafanikio kwa miaka minane mfululizo, kwa jumla kampuni kutoka nchi, maeneo na mashirika ya kimataifa zaidi ya 180 zimeshiriki kwenye maonesho hayo, mafanikio ya maonesho yameonekana dhahiri, na ushawishi wake unaendelea kupanua duniani.

Wafanyakazi wanaendelea kufanya mpangilio wa mabanda ndani ya Kituo cha Kitaifa cha Mikutano na Maonyesho (Shanghai) (picha ilipigwa tarehe 2 Novemba). (Xinhua/Ding Ting)

Wafanyakazi wanaendelea kufanya mpangilio wa mabanda ndani ya Kituo cha Kitaifa cha Mikutano na Maonyesho (Shanghai) (picha ilipigwa tarehe 2 Novemba). (Xinhua/Ding Ting)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha