Wajumbe wa "Kusini mwa Dunia" watafuta haki ya kutoa sauti kubwa zaidi katika Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Vyombo vya Habari Duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2026

Tarehe 6 Novemba 2026, mgeni anayeshiriki kwenye Mkutano wa Saba wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani akiangalia mkono wa roboti wenye ustadi katika Kituo cha Maonyesho cha Zhongguancun, Beijing, China. (Xinhua/Mao Zhu)

Tarehe 6 Novemba 2026, mgeni anayeshiriki kwenye Mkutano wa Saba wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani akiangalia mkono wa roboti wenye ustadi katika Kituo cha Maonyesho cha Zhongguancun, Beijing, China. (Xinhua/Mao Zhu)

Wakati AI inapojenga sura mpya ya sekta ya vyombo vya habari, wataalamu wenye uzoefu wa vyombo vya habari kutoka nchi za Kusini mwa Dunia wametoa wito wa kuimarisha ushirikiano katika Mkutano wa Saba wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani mjini Beijing, kwa lengo la kuongeza haki ya kutoa sauti kubwa zaidi za nchi zao katika utoaji habari duniani.

Mkutano huu umeandaliwa kwa pamoja na shirika la habari la China, Xinhua na Serikali ya Umma ya Mji wa Beijing, na umefanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Novemba. Mkutano huo umevutia wajumbe karibu 500 kutoka vyombo vya habari, jumuiya za washauri bingwa na idara za serikali kutoka nchi na maeneo 112, pamoja na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa.

Mkutano wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani ulianzishwa mwaka 2009, na kwa sasa umekuwa jukwaa muhimu la mawasiliano na ushirikiano kati ya viongozi na wataalamu wa vyombo vya habari linalovuka mipaka ya nchi na ya lugha.

Kenedid Ibrahim Houssein, Msimamizi Mkuu wa Uchapishaji wa gazeti la La Nation la Djibouti aliyehudhuria kwa mara ya kwanza kwenye mkutano huu alisema: "Umuhimu mkubwa wa mkutano huu ni kwamba umeshirikisha vyombo vya habari kutoka nchi mbalimbali duniani na kutupatia jukwaa la kujadili mustakabali wa sekta hii."

Aliongeza: "Tunatumaini kwa kupitia jukwaa hili tutaendeleza kwa kina uhusiano wa washirika kati yetu na China katika ubadilishanaji wa habari."

Agnes Kalekye Nguna, Mkurugenzi Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Kenya (Kenya Broadcasting Corporation), alisisitiza umuhimu wa kufanya mazungumzo kati ya ustaarabu kwenye msingi wa kuwa na usawa.

Alitoa wito wa kuchukua hatua zaidi za kupanua mawasiliano kati ya Afrika na China na kuendeleza kwa kina ushirikiano kati ya vyombo vya habari, akieleza kuwa uhusiano huo wa washirika wa kunufaishana na kutafuta maendeleo kwa pamoja unaweza kuwa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano kama huo katika Kusini mwa Dunia na maeneo mapana zaidi.

Katika Mkutano huo wenye kaulimbiu ya "Vyombo vya Habari katika Zama za AI: Kutoka Maoni ya Pamoja Hadi Vitendo", wajumbe wamejadili jinsi nchi za Kusini mwa Dunia zinavyoweza kushirikiana ili kusaidia vyombo vyao vya habari kuzoea teknolojia ya AI inavyotumiwa zaidi siku hadi siku katika sekta hii.

Siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita, Mkutano wa Saba wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani ulitoa "Pendekezo la Vyombo vya Habari Duniani kuhusu Kuandaa kwa Pamoja Vigezo vya Matumizi ya AI". Pendekezo hilo lililoanzishwa na shirika la habari la Xinhua linalenga kushirikisha vyombo vikubwa vya habari na mashirika mengine ya kitaalamu ili kwa pamoja kulinda ukweli wa habari, kuhakikisha usalama wa data na kufuata maadili ya vyombo vya habari, ili kudumisha imani ya umma kwa vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa pendekezo hilo, washiriki wanapanga kushirikiana kwa karibu katika kipindi cha takriban miaka miwili ijayo ili kuandaa mfumo wa kufuata vigezo unaohusisha hali mbalimbali za matumizi ya AI katika sekta ya vyombo vya habari na kukubaliwa pamoja na vyombo vya habari.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha