Watengenezaji magari wa China barani Afrika: kuunda mustakabali wa sekta ya magari

(CRI Online) Novemba 09, 2026

Mzamo Buthelezi

Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala wa Afrika Kusini Mzamo Buthelezi akihutubia Mkutano wa Africa Forward huko Johannesburg, Afrika Kusini Novemba 6, 2026. (Xinhua/Jiang Guopeng)

Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala wa Afrika Kusini Mzamo Buthelezi, amesema mpito wa kuelekea magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) unatoa fursa kubwa kwa bara la Afrika, lakini bara la Afrika linahitaji masuluhisho yanayoendana na mazingira ya ndani, yanayoweza kusaidia maendeleo mapana ya viwanda.

Buthelezi alisema hayo mjini Johannesburg kwenye hafla iliyofanyika kwenye mkutano wa Africa Forward, iliyoandaliwa na kampuni ya China inayotengeneza magari ya Jetour, ikiwakutanisha takriban wawakilishi 300 kutoka sekta ya magari, serikali, na sekta ya biashara ili kujadili mustakabali wa sekta ya magari barani Afrika.

Buthelezi alikaribisha mpango wa Jetour wa kuanza kutengeneza gari lake aina ya T2 katika kiwanda cha Rosslyn nchini humo ifikapo mwaka 2027, akieleza kuwa uwekezaji huo ni ishara thabiti ya imani kwa Afrika Kusini.

Ke Chuandeng, rais wa kampuni ya Jetour International, akitoa hotuba kwenye

Ke Chuandeng, rais wa kampuni ya Jetour International, akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Africa Forward huko Johannesburg, Afrika Kusini Novemba 6, 2026. (Xinhua/Jiang Guopeng)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha