Lugha Nyingine
Timu ya matibabu ya China yatoa huduma za afya bila malipo kwa zaidi ya wakazi 5,000 wa Tanzania Zanzibar
Timu ya 36 ya matibabu ya China iliyoko Tanzania Zanzibar, imekamilisha kazi yake ya siku nne ya kutoa huduma bila malipo katika Kituo cha Afya cha Kinduni, ikiwahudumia wakazi zaidi ya 5,000.
Kazi hiyo ilipangwa na Mfuko wa Maisha Bora unaoongozwa na mke wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi.
Kiongozi wa timu ya matibabu ya China Wang Wei amesema wataalamu wa China walishirikiana na wafanyakazi wa afya wenyeji kutoa huduma katika matengo mbalimbali.
Madaktari hao pia walibadilishana ujuzi wa uchunguzi na madaktari wa huko, na kuonesha mbinu za matibabu kazini, ushirikiano ambao Wang anasema, umechangia katika kuimarisha ujuzi wa kiufundi na uwezo wa kliniki wa wataalamu wa afya wa huko, na kugeuza shughuli moja kuwa fursa ya kuendeleza uwezo wa vituo vya afya katika ngazi ya shina.
Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla alikabidhi hati ya shukrani kwa timu hiyo ya madaktari.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



