Lugha Nyingine
Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China (4)
![]() |
| Tarehe 7 Novemba 2026, watu wakizungumza mbele ya ukuta wa waridi wa banda la Kenya kwenye Maonyesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China. (Xinhua/Chen Haoming) |
Ukuta wa waridi wenye urefu wa zaidi ya mita mbili kwenye banda la Kenya la Maonyesho ya 9 ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China (CIIE) uliwavutia watembeleaji wengi kusimama na kupiga picha. Kenya inatumaini kutumia fursa ya kushiriki kwenye maonyesho hayo kuleta harufu nzuri ya maua ya Kenya katika soko la China.
Kutokana na mazingira ya asili yenye hali nzuri ya kipekee, maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yanasifiwa sana kwa ubora wake na kiasi cha utoaji wake tulivu, na nchi hii siku zote inachukua nafasi ya mbele ya uuzaji wa nje wa maua mabichi barani Afrika katika muda mrefu uliopita.
Kenya ni moja ya nchi 53 za Afrika zinazonufaika kwanza na sera ya ushuru sifuri ya China, ambayo ilifanya kazi rasmi Tarehe mosi Mei mwaka huu. Hii imefanya mazao ya kilimo yenye umaalumu ya Afrika kuingia kwa urahisi zaidi katika soko la China, na kuimarisha imani ya wapandaji wa maua wa Kenya kwa uuzaji wa maua yao kwenye soko la China.
Kutoka Nyanda za Juu za Afrika Mashariki hadi soko la China, umbali kama unazidi kuwa mfupi zaidi, lakini mawasiliano yamekuwa ya karibu zaidi, na mwelekeo wa biashara pia umejitokeza zaidi. Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yanakaribia zama za dhahabu nchini China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




