Lugha Nyingine
Xi atoa wito wa kutukuza urithi wa Sun Yat-sen katika mchakato wa ustawishaji wa taifa

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia mkutano wa kuadhimisha miaka 160 tangu kuzaliwa kwa Sun Yat-sen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Novemba 12, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kutukuza urithi wa Sun Yat-sen, mmoja wa waasisi wa mapinduzi anayeheshimika sana, ili kufanya juhudi za pamoja za kufikia ustawishaji wa taifa na kuibadili kuwa hali halisi ndoto kuu ya watu wote wa China tokea zama za karibu.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo jana Alhamisi kwenye mkutano uliofanyika Beijing kuadhimisha miaka 160 tangu kuzaliwa kwa Sun.
Sun ambaye alizaliwa mwaka 1866, aliongoza Mapinduzi ya mwaka 1911 miaka zaidi ya mia moja iliyopita ili kukomesha mfumo wa kifalme wenye mamlaka yote ambao ulikuwa umetawala China kwa maelfu ya miaka. Sun alifariki dunia mwaka 1925.
Katika hotuba yake, Xi amemsifu Sun kuwa ni shujaa mkuu wa taifa, mzalendo mkuu, na mwanzilishi mkuu wa mapinduzi ya kidemokrasia ya China.
Amesema kuwa katika miaka zaidi ya 100 iliyopita, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeongoza watu wa China katika kuandika ukurasa tukufu zaidi katika historia ya taifa la China.
"Njia bora kwetu ya kumkumbuka Dkt. Sun ni kujifunza, kurithisha na kutukuza moyo wake wa thamani kubwa, kusukuma mbele kwa hatua madhubuti juhudi zetu za kujenga nchi yenye nguvu kubwa na kustawisha taifa letu," amesema Xi.
Xi amesisitiza kuwa kutatua suala la Taiwan na kufanikisha muungano kamili wa taifa ni jukumu la kihistoria lisilobadilika la Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ni matarajio ya pamoja ya watu wote wa China, na pia ni matakwa ya lazima ya ustawishaji mkubwa wa taifa la China.
Xi amesema watu katika pande zote mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan na Wachina wote ndani na nje ya nchi, wanapaswa kushirikiana katika kupinga nguvu za kutaka "Taiwan ijitenge", na kusukuma mbele kwa pamoja maendeleo ya amani ya uhusiano wa pande hizo mbili na kutimiza muungano kamili wa taifa.
"Kwenye msingi wa kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja na Makubaliano ya mwaka 1992, tunapenda kufanya mazungumzo na mashauriano na watu wenye maono na uelewa wa kina kutoka sekta mbalimbali za Taiwan juu ya masuala kuhusu uhusiano wa pande mbili za Mlango Bahari na muungano wa taifa," amesema Xi.
Xi amesema, "Tutazingatia vya kutosha hali halisi ya Taiwan na kutilia maanani vya kutosha maslahi na hisia za ndugu zetu huko Taiwan. Lakini kamwe hatutatoa nafasi yoyote kwa shughuli za mafarakano za kuifanya 'Taiwan ijitenge'."
"Mwelekeo wa historia ni usiozuilika. Muungano kamili wa taifa letu ni lazima utimie, na hakika unaweza kutimia," amesema Xi.

Mkutano wa kuadhimisha miaka 160 tangu kuzaliwa kwa Sun Yat-sen ukifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 12 Novemba 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia mkutano wa kuadhimisha miaka 160 tangu kuzaliwa kwa Sun Yat-sen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Novemba 12, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



