Lugha Nyingine
Washiriki wa COP31 wasema China inaingiza msukumo kwenye maendeleo ya kijani duniani

Watu wakitembelea Banda la China kwenye eneo la Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), jijini Antalya, Uturuki, Novemba 9, 2026. (Mustafa Kaya/kupitia Xinhua)
ANTALYA, Uturuki – Kwenye Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) unaoendelea Antalya, Uturuki, maofisa na wawakilishi kutoka serikalini na mashirika ya kimataifa wamesifu juhudi za China katika mabadiliko ya muundo wa maendeleo ya kijani, wakisema juhudi hizo zimeingiza msukumo kwenye maendeleo ya kijani duniani.
Wameyasema hayo baada ya kutolewa kwa toleo la Kiingereza la ripoti yenye kichwa cha "Mito ya Maji Safi na Milima ya Kijani Ndiyo Mali ya Dhahabu—Njia ya Maendeleo ya Kijani ya China” kwenye Banda la China la COP31 Jumanne wiki hii. Ripoti hiyo inalenga kuonesha kwa jumuiya ya kimataifa matarajio ya China juu ya maendeleo ya kijani, utekelezaji wake wa kihalisi, na umuhimu wake kwa dunia nzima.
Ripoti hiyo iliandaliwa kwa pamoja na timu ya watafiti katika Kituo cha Utafiti wa Fikra ya Xi Jinping juu ya Ustaarabu wa Ikolojia, Taasisi ya Xinhua, na Kituo cha Utafiti wa Maendeleo cha Idara ya Kitaifa ya Misitu na Mbuga ya China.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ya Asili (IUCN) Stewart Maginnis katika mahojiano yake na Shirika la Habari la China, Xinhua jijini Antalya, Uturuki ambao ni mwenyeji wa COP31 amesema, Dhana ya China ya Ustaarabu wa Ikolojia inaonesha kimsingi "maendeleo ya uchumi na ulinzi wa mazingira havihitaji kushindana, badala yake vinapaswa kwenda sambamba kwa kusaidiana."
Amesifu ahadi ya dhati ya China katika kulinda, kuhifadhi, na kurejesha mifumo ya ikolojia, akisisitiza kuwa chini ya matarajio ya kijani ya China, maliasili si tu zina thamani ya kimazingira, bali pia ni sehemu ya mfumo wa maendeleo wa nchi hiyo.
Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi, Simon Stiell, ameyaelezea mabadiliko ya muundo wa nishati wa China kuwa ni mafanikio yasiyo na mfano mahali pengine popote duniani," akisema mafanikio hayo yamechochea uvumbuzi na kupunguza gharama katika sehemu mbalimbali duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nishati Duniani (IEA), Fatih Birol, amesema kwenye mkutano huo kuwa China imepata mafanikio makubwa katika sekta ya magari yanayotumia umeme, nishati mbadala, na uhifadhi wa betri, akiongeza kuwa "China imeonesha njia kwa dunia."
Katika shughuli ya kutolewa kwa ripoti hiyo, Tennant Reed, msimamizi mkuu wa mabadiliko ya tabianchi na nishati katika Kundi la Viwanda la Australia, amekaribisha kutolewa kwa waraka huo wa ripoti, akisema ripori hiyo inaweza kuelezea vizuri zaidi uzoefu wa China wa maendeleo ya kijani.
Baada ya kutembelea China mara kadhaa kwa utalii na kushiriki kwenye semina za kitaaluma, Reed ameliambia Xinhua kwamba alivutiwa sana na mafanikio ya mabadiliko ya muundo wa kijani ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



