Putin aelezea msimamo wa Russia juu ya suluhisho la suala la Ukraine kwenye mazungumzo na wajumbe wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2026

Picha hii iliyotolewa na tovuti ya Kremlin ikimwonesha Rais wa Russia Vladimir Putin (wa kwanza, kulia) akikutana na mjumbe maalum wa Rais wa Marekani Donald Trump Steve Witkoff (wa pili, kushoto) na mkwe wa Trump Jared Kushner (wa kwanza, kushoto) mjini Moscow, Russia, Nov. 12, 2026. (Ofisi ya Habari ya Kremlin/kupitia Xinhua)

MOSCOW - Rais wa Russia Vladimir Putin amekutana na wajumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner mjini Moscow jana Alhamisi, akisisitiza upingaji wa Kremlin dhidi ya kutumwa kwa vikosi vya wanajeshi wa kigeni nchini Ukraine.

Witkoff ameelezea matumaini yake kuwa mkutano huo utafungua njia kwa ajili ya duru mpya ya mazungumzo ya pande nyingi yanayohusisha wawakilishi wa Ulaya.

Putin amesema uwepo wa wanajeshi wowote wa kigeni katika ardhi ya Ukraine hautakubalika kabisa kwa Russia, kwani itatishia usalama wa taifa la Russia. Ameonya kwamba wanajeshi wa namna hiyo watachukuliwa kuwa watu halali wa kulengwa na vikosi vya Russia.

Putin amesema ni muhimu kusikia tathmini ya Witkoff kuhusu mazungumzo ya hivi karibuni ya pande tatu huko Abu Dhabi na matarajio ya mazungumzo zaidi kati ya Russia na Ukraine, haswa kutoka mtazamo wa Ulaya, kutokana na kuwepo kwa mawasiliano ya Witkoff na wawakilishi wa Ulaya.

Kuhusu masuala ya ardhi, Putin amesema pendekezo la upande wa Ukraine kuhusu kile kinachoitwa "maeneo ya rangi ya kijivu" (gray zones) linaweza kusababisha migogoro na kudhoofisha makubaliano yoyote.

Amesisitiza kuwa Russia itatambua tu mpaka wa nchi kama mstari wa kutenganishwa na Ukraine, akionya kwamba majadiliano kuhusu "maeneo ya rangi ya kijivu" yanaweza kusababisha tafsiri tofauti na kutokukubaliana.

Witkoff amesema Rais wa Marekani Donald Trump alimtaka aeleze umuhimu wa kumaliza mgogoro nchini Ukraine mapema iwezekanavyo.

Kushner amesema anatumai mkutano huo utatoa fursa ya kutafuta njia zinazowezekana za kumaliza mgogoro huo. Ameongeza kuwa wawakilishi wa Ulaya wameonesha nia ya kushiriki katika mazungumzo na kusaidia kuleta amani ya kudumu.

Duru ya Mazungumzo ya siku mbili ya pande tatu yaliyohusisha Russia, Marekani na Ukraine yalimalizia juzi Jumatano huko Abu Dhabi, mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu. Pande hizo zilifikia makubaliano juu ya kubadilishana kwa idadi kubwa wafungwa wa vita lakini zimeendelea kugawanyika kwa kina juu ya masuala muhimu, yakiwemo ya kumaliza mgogoro huo, mitafaruku ya ardhi, mahakikisho ya usalama kwa Ukraine na mfumokazi wa usalama wa baadaye wa Ulaya.

Picha hii iliyotolewa na tovuti ya Kremlin ikimwonesha Rais wa Russia Vladimir Putin (wa kwanza, kulia) akikutana na mjumbe maalum wa Rais wa Marekani Donald Trump Steve Witkoff (wa pili, kushoto) na mkwe wa Trump Jared Kushner (wa kwanza, kushoto) mjini Moscow, Russia, Nov. 12, 2026. (Ofisi ya Habari ya Kremlin/kupitia Xinhua)

Picha hii iliyotolewa na tovuti ya Kremlin ikimwonesha Rais wa Russia Vladimir Putin (wa nne, kulia) akikutana na mjumbe maalum wa Rais wa Marekani Donald Trump Steve Witkoff (wa pili, kushoto) na mkwe wa Trump Jared Kushner (wa kwanza, kushoto) mjini Moscow, Russia, Nov. 12, 2026. (Ofisi ya Habari ya Kremlin/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha