Lugha Nyingine
China na wanachama wengine wa APEC zatimiza matunda takriban 50 ya kivitendo katika uchumi na biashara mwaka huu

Li Chenggang (katikati), Mwakilishi wa Biashara ya Kimataifa wa China ambaye pia ni Naibu Waziri wa Biashara, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye kituo cha vyombo vya habari cha Wiki ya Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) 2026, mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, tarehe 16 Novemba 2026. (Xinhua/Bai Xueqi)
SHENZHEN - Wizara ya Biashara ya China imesema kuwa, China imeshirikiana na wanachama wengine wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) kutimiza matunda takriban 50 ya kivitendo katika uchumi na biashara mwaka huu.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Shenzhen, mji mwenyeji wa mkutano huo, jana Jumatatu, Li Chenggang, Mwakilishi wa Biashara ya Kimataifa wa China ambaye pia ni Naibu Waziri wa Biashara wa China, amesema tangu mwanzo wa mwaka huu, wizara hiyo imeshirikiana na idara husika ili kuhimiza ushirikiano katika kuendeleza ujumuishi wa kiuchumi wa kikanda.
Aidha, amesema wizara hiyo imefanya kazi na idara hizo kuunga mkono kazi za Shirika la Biashara Duniani (WTO), kuzidisha ushirikiano katika nyanja za kidijitali na mambo ya teknolojia ya AI, na kuendeleza uchumi wa kijani.

Picha iliyopigwa tarehe 16 Novemba 2026 ikionesha mkutano na waandishi wa habari kwenye kituo cha vyombo vya habari kwa ajili ya Wiki ya Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) 2026, mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. (Xinhua/Bai Xueqi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



