Cote d'Ivoire na Botswana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2026

Rais wa Botswana, Duma Gideon Boko, akitoa hotuba jijini Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire, Novemba 16, 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Rais wa Botswana, Duma Gideon Boko, akitoa hotuba jijini Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire, Novemba 16, 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

ABIDJAN - Cote d'Ivoire na Botswana zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa pande mbili, hasa katika uchimbaji madini, nishati, kilimo na biashara, kufuatia mazungumzo kati ya Rais wa Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara, na mwenzake wa Botswana, Duma Gideon Boko, jijini Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire jana Jumatatu.

Ouattara ameyaelezea mazungumzo hayo kuwa "yenye tija na ya kirafiki," akibainisha kuwa kiwango cha sasa cha biashara kati ya nchi hizo mbili hakiakisi uwezo wao wa kiuchumi. Ametoa wito kwa sekta binafsi ya Botswana kuongeza uwekezaji nchini Cote d'Ivoire, hasa katika uchimbaji madini, petroli, na miradi mikubwa ya maendeleo.

Boko, ambaye yuko katika ziara ya kitaifa nchini humo kuanzia Jumapili hadi Jumatano wiki hii, amesisitiza umuhimu wa kuufanya uchumi wa nchi zote mbili kuwa wa kutegemea sekta mbalimbali kwa kutumia vyema rasilimali asili na za madini, ardhi ya kilimo, na idadi ya vijana.

Nchi hizo mbili pia zimetia saini nyaraka kadhaa za maelewano siku hiyo ya Jumatatu, zinazohusu uchimbaji madini, nishati, mambo ya kiuchumi, diplomasia, na afya ya binadamu na wanyama.

Boko atahudhuria jukwaa la uchumi la Cote d'Ivoire na Botswana leo Jumanne na ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Rasilimali za Kuchimbwa na Nishati kesho Jumatano, ambapo Botswana itakuwa nchi mgeni wa heshima. 

Rais wa Botswana Duma Gideon Boko (kushoto), na Rais wa Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara, wakitoa hotuba baada ya mkutano wao jijini Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire, Novemba 16, 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Rais wa Botswana Duma Gideon Boko (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara jijini Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire, Novemba 16, 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha