Xi asema kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Canada ni chaguo sahihi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2026

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, ambaye yuko nchini China kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), mjini Shenzhen, katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Novemba 17, 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping amesema kuwa kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Canada ni chaguo sahihi linalolingana na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na kusaidia amani, utulivu, maendeleo na ustawi duniani.

Xi ameyasema hayo jana Jumanne mjini Shenzhen wakati akikutana na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney ambaye yuko Shenzhen kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), ambao utafanyika kuanzia leo tarehe 18 hadi kesho tarehe 19 Novemba.

"Katika miaka mingi iliyopita maendeleo ya uhusiano kati ya China na Canada yameonesha kuwa, ni muhimu sana kuheshimiana, kuwa na usawa na kunufaishana, na kutafuta maoni ya pamoja wakati wa kuweka kando maoni tofauti," amesema Xi, akiongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Canada katika kusukuma mbele uhusiano mpya wa washirika wa kimkakati.

Amesema nchi hizo mbili zinapaswa kufanya vizuri zaidi uratibu na kufanya juhudi za kuendeleza kwa kina ushirikiano katika sekta za jadi za biashara, nishati, kilimo na mambo ya fedha, na wakati huo huo kupanua ushirikiano katika maeneo mapya yanayoibukia, kama vile uchumi wa kijani, biashara ya mtandaoni na uchumi wa kidijitali, ili kutumia vizuri zaidi nguvu bora za kila upande na kufikia matokeo yenye manufaa kwa pande zote mbili.

Pia amependekeza kuongeza uratibu, kufanya uzoefu kwa pamoja katika ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kushikilia mamlaka na heshima ya Umoja wa Mataifa na mfumo wa biashara wa pande nyingi, na kujenga mfumo wa usimamizi wa dunia ulio wa usawa na haki zaidi.

Kwa upande wake Carney amesema kuwa uhusiano wa nchi mbili siku zote unaendelea kwenye njia sahihi ya maendeleo tangu kuanzishwa kwa uhusiano mpya wa washirika wa kimkakati kati ya Canada na China wakati wa mkutano wake na Xi mwanzoni mwa mwaka huu.

"Nchi hizi mbili zinaweza kusukuma mbele vya kutosha na kuendeleza kwa kina ushirikiano kati yao kwenye msingi wa kuheshimiana," amesema Carney. Amesema Canada itashirikiana na China ili kutafuta ushirikiano wa karibu zaidi katika biashara, uwekezaji, nishati mpya, mazao kilimo, AI, utalii na maeneo mengine, kupunguza hali zinazoleta mikwaruzano, na kupanua orodha ya mambo ya ushirikiano.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, ambaye yuko nchini China kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), mjini Shenzhen, katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Novemba 17, 2026. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha