Lugha Nyingine
Xi asema kuendeleza uhusiano wa China-Mexico ni muhimu kwa nchi za Kusini mwa Dunia katika kutafuta nguvu kupitia mshikamano

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum Pardo, ambaye yuko nchini China kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, Novemba 17, 2026. (Xinhua/Shen Hong)
SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping amesema kuwa kuendeleza uhusiano kati ya China na Mexico hadi ngazi mpya, katika maeneo mapana zaidi na kwa kina zaidi kuna umuhimu mkubwa katika kutekeleza mikakati ya maendeleo ya kila nchi kati yao pamoja na kuunga mkono nchi za Kusini mwa Dunia katika kutafuta nguvu kupitia mshikamano.
Xi ameyasema hayo jana Jumanne wakati akikutana na Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum Pardo ambaye yuko Shenzhen, China kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), ambao utafanyika kuanzia leo Novemba 18 na kumalizika kesho Alhamisi Novemba 19.
Xi ametoa wito wa kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa kati ya China na Mexico, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kwenye ngazi mbalimbali, kushikilia kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kutafuta maendeleo kwa pamoja, kuimarisha hali ya kuhusishana na kuungana mkono katika mkakati, na kuzidisha ushirikiano katika miundombinu, sayansi na teknolojia, nishati safi, utamaduni na utalii.
Amesisitiza kuwa pande zote mbili zinatakiwa kushikilia usawa na haki, kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi, kuongeza uratibu kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa na majukwaa mengine ya pande nyingi, na kulinda kanuni za kimsingi za kulinda uhusiano wa kimataifa.
Pia, Xi ametoa wito wa kuendeleza kwa kina ushirikiano kati ya China na nchi za Latini Amerika na Karibiani (LAC), na kujenga pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja kupitia kuhimiza utekelezaji wa miradi mitano ya jumuiya ya China na LAC.
Kwa upande wake Sheinbaum, ameeleza kuwa Mexico na China zimekuwa na urafiki mkubwa, zina mawazo yanayofanana kuhusu maendeleo, na zimepata matunda mengi katika ushirikiano katika sekta mbalimbali, amesema Mexico iko tayari kupanua ushirikiano na China katika biashara, uwekezaji, sayansi na teknolojia, viwanda vya utengenezaji bidhaa, na AI, wakati huohuo kuhimiza mawasiliano katika sekta za afya, elimu, utamaduni, na utalii.
Sheinbaum amesema Mexico iko tayari kufanya ushirikiano na China kila wakati, kuimarisha uratibu wa pande nyingi, kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi za Kusini mwa Dunia.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum Pardo, ambaye yuko nchini China kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, Novemba 17, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma