Lugha Nyingine
Xi Jinping amkaribisha Trump katika uwanja wa ndege wa Shenzhen

Rais wa China Xi Jinping akimkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bao' an wa Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)
SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping amemkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bao' an wa Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China jana Jumatano.
Trump yuko mjini Shenzhen kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), unaofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 19 Novemba.
Huku muziki wa makaribisho ukisikika, Xi Jinping na Trump walishikana mikono kwa uchangamfu. Askari wa gwaride la heshima wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) walitoa saluti ya silaha, na binti mmoja alimkabidhi kiongozi huyo wa Marekani shada la maua.
Bendera za taifa za China na Marekani zilikuwa zikipepea upeponi wakati bendi ya jeshi ikipiga nyimbo za taifa za nchi hizo mbili, na ndege za kivita ziliruka angani kutoa saluti. Viongozi hao wawili wa nchi walilipungia mkono kundi la vijana lililoshiriki hafla hiyo ya makaribisho.
Xi amekumbuka ziara yake ya kiserikali nchini Marekani mwezi Septemba mwaka huu, ambapo Rais wa Marekani na mkewe walifika wenyewe katika uwanja wa ndege na kuandaa hafla kubwa ya mapokezi, akieleza kuwa China ni nchi inayofuata maadili ya jadi, na inatilia maanani kulipa wema kwa wema.
Akimkaribisha Trump kufanya ziara nchini China kwa mara nyingine tena, Xi amesema anatarajia kubadilishana maoni kwa kina na Rais wa Marekani kuhusu uhusiano wa pande mbili, ushirikiano wa Asia-Pasifiki, na hali ya hivi sasa ya dunia nzima na masuala mengine makubwa ili kuendeleza uhusiano wa kiujenzi wa China-Marekani ulio wa utulivu wa kimkakati kwenye msingi wa kuheshimiana, kuwa na usawa na kunufaishana.
Trump amemshukuru Xi kwa kumlaki yeye mwenyewe katika uwanja wa ndege na kwa maandalizi maalum yaliyofanywa na upande wa China. Amesema ana furaha kubwa kutembelea China kwa mara nyingine tena, akiita China kuwa ni nchi kubwa na Xi kuwa ni kiongozi mahiri.
Trump amesema kuwa kila mkutano wake na Xi umekuwa wa kufurahisha sana, na anaamini kuwa ziara yake hiyo itasukuma mbele zaidi maendeleo ya uhusiano wa pande mbili na kupata mafanikio kamili.

Rais wa China Xi Jinping akimkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bao' an wa Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akimkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bao' an wa Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais wa China Xi Jinping akimkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bao' an wa Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma