Xi Jinping aandaa dhifa ya kukaribisha wageni wanaohudhuria mkutano wa APEC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2026

Rais wa China Xi Jinping akizungumza kwenye dhifa ya kukaribisha wageni huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping na mkewe, Peng Liyuan wameandaa dhifa huko Shenzhen kuwakaribisha wageni ambao wako katika mji huo kuhudhuria Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC).

"Kwa niaba ya serikali ya China na watu wa China, ninawakaribisha kwa furaha kubwa zaidi wageni wote waheshimiwa," alisema Xi kwenye hotuba yake fupi ya ukaribisho.

"Ufunguaji mlango umejikita mizizi kwa kina katika jeni ya Shenzhen na uvumbuzi unasukuma nguvuhai za mji huu, na ushirikiano ndiyo chanzo cha nguvu ya mji huu," amesema Xi, akiongeza kuwa mafanikio ya Shenzhen pia ni kielelezo cha mageuzi na ufunguaji mlango wa China, vilevile mfano wa ushirikiano wenye matunda katika eneo la Asia-Pasifiki.

Xi amedhihirisha kuwa ufunguaji mlango, uvumbuzi na ushirikiano vimekuwa sifa za kipekee za APEC tangu kuanzishwa kwake, na APEC imeweza kufuata mwelekeo wa nyakati na kuongoza mchakato wa mtangamano wa kiuchumi wa kikanda, hali ambayo imeifanya Asia-Pasifiki kuwa eneo lenye nguvu hai zaidi ya maendeleo, na injini muhimu ya kujipatia ongezeko la uchumi duniani."

"Kwenye Mkutano wa Viongozi utakaofanyika kesho (leo), tutajadili hatua za kupanua kufunguliana milango, kutafuta njia ya kujipatia ongezeko la uchumi kwa kutegemea msukumo wa uvumbuzi, na kuongeza fursa kwa ushirikiano wenye mwelekeo wa matokeo katika sekta mbalimbali," amesema Xi.

Kabla ya dhifa hiyo iliyofanyika jana Jumatano jioni, Xi na Peng walipiga picha pamoja na viongozi na wawakilishi kutoka nchi na maeneo wajumbe wa APEC na wake zao.

Baada ya dhifa hiyo, walitazama pamoja na wageni hao maonesho ya sanaa.

Rais wa China Xi Jinping akizungumza kwenye dhifa ya kukaribisha wageni huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na wageni huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akizungumza na Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump kabla ya dhifa ya kukaribisha wageni huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum Pardo akiwasili kuhudhuria dhifa ya kukaribisha wageni kwenye Kituo cha Mawasiliano ya Kimataifa cha Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Waziri Mkuu wa Papua New Guinean James Marape akiwasili kuhudhuria dhifa ya kukaribisha wageni kwenye Kituo cha mawasiliano ya Kimataifa cha Shenzhen, tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung na mkewe wakiwasili kuhudhuria dhifa ya kukaribisha wageni kwenye Kituo cha mawasiliano ya Kimataifa cha Shenzhen, tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon akiwasili kuhudhuria dhifa ya kukaribisha wageni kwenye Kituo cha Mawasiliano ya Kimataifa  cha Shenzhen  tarehe 18 Novemba 2026. (Xinhua/Ding Lin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha