Xi aongoza mkutano wa kwanza wa kihistoria wa marais wa China, Russia na Marekani akiwa pamoja na Putin na Trump

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2026

Rais wa China Xi Jinping akiwa pamoja na  Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump wamefanya mkutano wa wakuu wa China, Russia na Marekani huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 19 Novemba, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping ameongoza mkutano wa kihistoria wa viongozi mjini Shenzhen, akiwa pamoja na Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump, ambao ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya viongozi wakuu hao wa nchi za China, Russia na Marekani.

Kwenye mkutano huo wa jana Alhamisi viongozi hao watatu walibadilishana maoni kwa kina kuhusu hali ya hivi sasa ya kimataifa na wakiahidi kudumisha utulivu wa kimkakati na usalama wa kimataifa.

Baada ya mkutano huo kumalizika, nchi hizo tatu zilitoa " Tangazo la Amani la Viongozi Wakuu wa China, Russia na Marekani," likielezea maelewano yao ya pamoja kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mageuzi ya Umoja wa Mataifa, usalama wa nishati, mamlaka ya Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC), na kupunguza hatari za silaha za nyuklia.

Xi ameuelezea mkutano huo wa pande tatu kuwa ni wenye umuhimu wa kihistoria . Amesema kuwa amani kati ya nchi kubwa inaweza kuleta utulivu kwa dunia, wakati migogoro kati yao inaweza tu kusababisha machafuko.

“Amani ni utafutaji wa binadamu wa siku zote bila kulegea ” amesema Xi, huku akieleza kuwa dunia imepita vita zaidi ya 10,000, na hivi sasa migogoro zaidi ya 60 bado inaendelea katika sehemu mbalimbali duniani.

Xi ametoa maoni yake ya pointi nne kuhusu namna nchi kubwa zinaweza kupata njia sahihi ya kutendeana na kulinda kwa pamoja amani ya dunia . Ametoa wito wa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kufanya mazungumzo na mashauriano.

Kwa mujibu wa tangazo hilo la pande hizo tatu, viongozi hao wakuu wamesisitiza tena kuwa vita vya nyuklia hakuna anayeweza kuvishinda na kamwe havipaswi kupiganwa. Nchi hizo tatu zitafanya mazungumzo kuhusu kupunguza hatari za silaha za nyuklia na kuzuia silaha za nyuklia zisienee.

Kwa upande wake, Putin amesema kuwa Russia inapenda kushirikiana na China na Marekani katika kuhimiza biashara ya kimataifa iliyo huria na wazi, kulinda usalama wa nishati na chakula, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika usimamizi wa AI.Trump amesema kuwa Marekani, China, na Russia, zikiwa nchi zenye nguvu za nyuklia, zinabeba wajibu mkubwa maalum wa kudumisha amani na utulivu duniani.

Viongozi hao watatu pia wamebadilishana maoni kuhusu masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, ikiwemo pamoja na msukosuko wa Ukraine, kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia, hali ya Mashariki ya Kati na hali ya peninsula ya Korea.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano wa  wakuu wa China, Russia na Marekani akiwa pamoja na Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump huko Shenzhen mkoani Guangdong, kusini mwa China, tarehe 19 Novemba, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano wa wakuu wa China, Russia na Marekani akiwa pamoja na Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Shenzhen tarehe 19 Novemba, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mkutano wa wakuu wa China, Russia na Marekani akiwa pamoja na Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Shenzhen, tarehe 19 Novemba, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha