Xi akutana na Trump, akitoa wito wa juhudi za kuelekeza uhusiano wa China na Marekani kufuata njia sahihi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2026

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alikuwa nchini China kuhudhuria kwenye Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), mjini Shenzhen, katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Novemba 19, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Marekani Donald Trump jana Alhamisi mjini Shenzhen, akitoa wito wa kuendelea na juhudi za kuelekeza kwa pamoja meli kubwa ya uhusiano kati ya China na Marekani kufuata mwelekeo sahihi wa kuelekea siku za baadaye.

Trump alikuwa nchini China kuhudhuria kwenye Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), uliofanyika Novemba 18-19 mjini Shenzhen, kusini mwa China.

Katika wakati wa mkutano huo, Xi amesema kuwa uhusiano kati ya China na Marekani umedumisha mwelekeo tulivu na wa kuhimiza hamasa katika hali ya jumla, ukileta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizi mbili na kuingiza hali ya utulivu na uhakika duniani.

Xi amesema yeye na Trump wamejadili na kutafuta kwa pamoja njia sahihi ya kutendeana kati ya nchi kubwa mbili za China na Marekani, wametoa matarajio mapya ya kujenga uhusiano wa kiujenzi wenye utulivu wa kimkakati kati ya China na Marekani, na kuupa uhusiano huo maudhui mapya yenye msingi wa kuheshimiana, kuwa na usawa na kunufaishana.

"Matarajio hayo mapya yamekaribishwa na watu wa China na Marekani, vilevile jumuiya ya kimataifa," ameongeza.

Pande zote mbili zimekubaliana kuandaa mpango mtendaji kwa ajili ya kuhimiza kiujenzi uhusiano wenye utulivu wa kimkakati kati ya China na Marekani.

Kuhusu suala la Taiwan, Xi amesema, upande wa Marekani unapaswa kuendelea kufanya jambo sahihi na kuepuka na matatizo makubwa kutokea katika uhusiano kati ya China na Marekani.

Trump amesema yeye na Xi wameongoza kwa pamoja maendeleo ya uhusiano kati ya Marekani na China, akiongeza kuwa viongozi wote wawili wamedumisha mawasiliano ya karibu, na urafiki wao unazidi kuimarika.

Trump ameeleza kuwa "Mawasiliano ya biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili yanaendelea kuongezeka, na ushirikiano katika dawa ya fentanyl na masuala mengine pia umeleta matokeo," Trump amebainisha.

Amehimiza pande zote mbili kufuata mwelekeo wa kuhimiza juhudi za kudumisha maendeleo tulivu ya uhusiano wa pande mbili na kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya mazao ya kilimo, nishati, na AI.

Marekani haiungi mkono "Taiwan ijitenge," Trump amesema.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alikuwa nchini China kuhudhuria kwenye Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), mjini Shenzhen, Novemba 19, 2026. (Xinhua/Li Tao)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alikuwa nchini China kuhudhuria kwenye Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), mjini Shenzhen, Novemba 19, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha