Xi Jinping aongoza mkutano wa APEC, atoa wito wa kujenga jumuiya ya Asia-Pasifiki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2026

Rais wa China Xi Jinping akiongoza Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) na kutoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kujenga Jumuiya ya Asia-Pasifiki na Kuandika Ukurasa Mpya wa Muujiza wa Asia-Pasifiki" mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Novemba 19, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping jana Alhamisi wakati akiongoza Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) uliofanyika mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China kuanzia Novemba 18 hadi 19, ametoa wito wa kuongeza juhudi zaidi za kujenga jumuiya ya Asia-Pasifiki na kuandika ukurasa mpya wa "muujiza wa Asia-Pasifiki."

"Lazima tujitahidi kujenga jumuiya ya Asia-Pasifiki yenye sifa za mshikamano na kusaidiana, ufunguaji mlango na ushirikiano, ujasiriamali na uvumbuzi, vilevile maendeleo jumuishi," amesema Xi katika hotuba yake hiyo yenye kichwa cha "Kujenga Jumuiya ya Asia-Pasifiki na Kuandika Ukurasa Mpya wa Muujiza wa Asia-Pasifiki"

Xi amebainisha kuwa kwa miongo zaidi ya mitatu, eneo la Asia-Pasifiki limepitia mabadiliko makubwa, na kutengeneza "muujiza wa Asia-Pasifiki" wa ukuaji wa haraka wa uchumi.

"Katika kukabiliana na fursa na changamoto mpya, eneo hili lazima libadilike kuendana na uhalisia mpya na kufungua matarajio mapya kwa ajili ya ushirikiano wa Asia-Pasifiki," ameongeza.

Xi ametoa wito wa mshikamano na kusaidiana katika kujenga jumuiya ya Asia-Pasifiki, akihimiza wanachama wa APEC kupanua maslahi yao ya pamoja, kukabiliana na mambo magumu na changamoto kwa pamoja, na kwa kasi tulivu kujenga hisia ya pamoja ya kuwa jumuiya.

"Wanachama wa APEC ni kama abiria wanaosafiri ndani ya meli moja. Ili kuvuka mawimbi ya Bahari ya Pasifiki, lazima tuungane na kujaliana," amesema.

Kujenga jumuiya ya Asia-Pasifiki kunahitaji ujasiriamali na uvumbuzi, Xi amesema, akihimiza ushirikiano imara zaidi katika sayansi na teknolojia, kubadili matokeo ya uvumbuzi kuwa biashara, na kujenga mazingira yaliyo ya wazi, haki, usawa na yasiyo ya kibaguzi kwa ajili ya ushirikiano.

Pia amesisitiza umuhimu wa maendeleo jumuishi, akisisitiza haja ya kuhakikisha kuwa maendeleo yananufaisha wote, yanatoa matokeo kwa watu, na kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya kubadilisha maono ya jumuiya ya Asia-Pasifiki kuwa uhalisia.

APEC iliyoanzishwa mwaka 1989, kwa sasa inajumuisha nchi na maeneo wanachama 21, ikiwemo China, Russia, na Marekani. China ilijiunga mwaka 1991. Jukwaa hili limesaidia kupanua biashara na uwekezaji, na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi katika eneo hilo.

"China imekuwa mtetezi, mhamasishaji, na mstari wa mbele katika ushirikiano wa kiuchumi wa Asia-Pasifiki," amesema Xi kwenye mkutano huo wa Shenzhen, akiongeza kuwa nchi hiyo iko tayari kushirikiana na pande zote kujenga nguzo nne muhimu za jumuiya ya Asia-Pasifiki — uchumi na biashara, muunganisho, uvumbuzi, na maendeleo.

Viongozi na wawakilishi wa nchi na maeneo wanachama wa APEC walitoa maoni yao kwenye mkutano huo juu ya kujenga jumuiya ya Asia-Pasifiki ili kufikia ustawi wa pamoja.

Walizungumza kwa kusifia sana mafanikio ya China ya kuwa mwenyeji wa APEC mwaka huu, na wameeleza utayari wao wa kuongeza ushirikiano ili kusukuma mbele maendeleo ya APEC.

Katika hotuba yake ya kufunga mkutano huo, Xi ametoa wito wa kuimarisha imani ili kubadilisha makubaliano juu ya ujenzi wa jumuiya ya Asia-Pasifiki kuwa vitendo halisi, na kubadili maono hayo kuwa uhalisia.

Mkutano huo umepitisha kwa kauli moja Azimio la Viongozi wa APEC 2026, ambalo linatoa Mtazamo wa Shenzhen juu ya ujenzi wa jumuiya ya Asia-Pasifiki, pamoja na nyaraka tatu juu ya biashara, muunganisho, na uvumbuzi.

Vietnam imechukua nafasi ya kuwa mwenyeji wa zamu wa APEC kwa mwaka 2027, na Rais To Lam amewaalika viongozi na wawakilishi wa nchi na maeneo wanachama kuhudhuria mkutano wa mwaka ujao nchini Vietnam.

Rais wa China Xi Jinping akipiga picha ya kundi na viongozi pamoja na wawakilishi kutoka wanachama wengine, kabla ya Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, tarehe 19 Novemba, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais wa China Xi Jinping akiongoza Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) na kutoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kujenga Jumuiya ya Asia-Pasifiki na Kuandika Ukurasa Mpya wa Muujiza wa Asia-Pasifiki" mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Novemba 19, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha