Lugha Nyingine
Marais wa Uganda na Tanzania wazindua kiwanda cha kuunganisha magari kilichowekezwa na China

(Picha/Xinhua)
Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania aliyekuwa ziarani nchini Uganda, wamezindua kwa pamoja kiwanda cha kuunda magari kilichowekezwa na China chenye thamani ya dola milioni 30 katikati ya Uganda, wakionyesha juhudi za kuendeleza maendeleo ya viwanda na uwezo wa utengenezaji wa kikanda.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Uganda imesema kiwanda cha Double Q Automotive Assembly, kilichopo Wilaya ya Mpigi, kina uwezo wa kuunda malori 4,000 kwa mwaka na kinaajiri zaidi ya Waganda 1,200.
Kituo hicho kinaunda malori mazito na kinatarajiwa kuimarisha uwezo wa utengenezaji wa magari wa Uganda, kuleta nafasi za ajira na kuimarisha ushirikiano wa viwanda na biashara kati ya Uganda na Tanzania.
Rais Museveni amewataka wawekezaji kuimarisha uhusiano na wazalishaji wa chuma wa ndani, ili kuhimiza uongezaji thamani wa ndani na kupunguza utegemezi wa vifaa vinavyoagizwa kutoka nje.

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma