TISCO na Huawei zashirikiana kuendeleza mabadiliko ya kidijitali nchini Kenya

(CRI Online) Novemba 23, 2026

Kampuni ya mashine za ujenzi ya TISCO na Huawei hivi karibuni walifanya kongamano la pamoja jijini Nairobi ili kuchunguza ushirikiano wa kidijitali kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa uendeshaji na kuboresha huduma kwa wateja.

Kongamano hilo lenye kaulimbiu "Kuimarisha Huduma na Uzoefu kwa Wateja," liliwaleta pamoja washirika wa sekta na wawakilishi wa makampuni ili kujadili namna teknolojia za kidijitali zinavyoweza kusaidia mabadiliko na maboresho ya viwanda vya jadi.

Shi Qinghua, mkurugenzi mkuu wa Huawei Cloud Kenya, amesema Huawei itatoa masuluhisho ya kidijitali na miundombinu ya wingu ili kusaidia mabadiliko ya kidijitali ya TISCO. Alibainisha kuwa Huawei itaendelea kurekebisha teknolojia zake kutokana na mahitaji ya kienyeji, kuwezesha uhamishaji wa maarifa na kujenga mfumo ikolojia endelevu wa kidijitali ambao haumwachi mtu yeyote nyuma.

Naye mwenyekiti wa kampuni ya TISCO, Zhang Yuanxiang, amesema kuwa ushirikiano na Huawei utasaidia juhudi za kampuni hiyo katika mabadiliko ya kidijitali. Amesisitiza kuwa biashara katika sekta za jadi zinahitaji teknolojia na zana kutoka kampuni za teknolojia ya juu ili kuboresha viwango vyake vya usimamizi na uwezo wa kutoa huduma kwa wateja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha