Timu ya madaktari wa China yafanya huduma ya matibabu kwa umma visiwani Zanzibar, Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 23, 2026

Madaktari wa Timu ya 36 ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania wakifanya shughuli ya huduma ya afya kwa umma kwenye Kituo cha Watoto Yatima cha Kitumba katika Kisiwa cha Unguja, Zanzibar, Tanzania, Novemba 21, 2026. (Timu ya 36 ya Madaktari ya China visiwani Zanzibar, Tanzania/kupitia Xinhua)

DAR ES SALAAM - Timu ya 36 ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania ilifanya shughuli ya huduma ya afya kwa umma kwenye Kituo cha Watoto Yatima cha Kitumba katika Kisiwa cha Unguja, Zanzibar, Tanzania siku ya Jumamosi.

Kiongozi wa timu hiyo Wang Wei amesema, shughuli hiyo ni sehemu ya mpango wa China wa "Timu 100 za Madaktari katika Vijiji 1,000", na ilifanyika kuadhimisha Siku ya Watoto Duniani.

"Shughuli hiyo ilihusisha mafunzo ya elimu ya afya katika lugha mbili za Kiingereza na Kiswahili. Kwa kutumia vifaa vya kuonesha na michezo shirikishi, madaktari waliwafundisha watoto kuhusu utunzaji wa meno na macho," Wang amesema, akiongeza kuwa mafunzo hayo yanaweza kusaidia watoto kujifunza na kukumbuka mwongozo wa afya haraka.

Wang amesema, wataalamu wa magonjwa ya ndani, upasuaji, ENT, stomatoloji, ophthalmoloji, na radiolojia walitoa huduma za kupima mwili na uchunguzi wa tumbo kwa kutumia ultrasound kwa watoto wote. Amesema, timu hiyo ilitayarisha faili za afya za kibinafsi, pamoja na kuweka kumbukumbu za ufuatiliaji kwa matatizo ya kuharibika kwa meno, uoni usio wa kawaida, utapiamlo, na hali zingine.

Wang amsema, "Mfumo wa rufaa umeanzishwa na wafanyakazi wa kituo hicho cha yatima ili kufuatilia na kutoa huduma ya kila mara kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Timu hiyo pia iliwapa vifaa vya steshenari, vitabu vya picha, mipira ya kandanda na wanasesere kabla ya kujiunga na watoto katika kuchora na kufanya michezo.”

Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Kitumba, Idrisa Juma Kombo, amesema ni nadra watoto hao kupata huduma ya upimaji wa hali ya afya.

Madaktari Wachina si tu wamegundua matatizo ya afya ya watoto bali pia wamechangia ujuzi wa usafi unaoweza kuwasaidia watoto. Watoto walikuwa na furaha kubwa na watakumbuka nyuso tabasamu za kikunjufu za madaktari Wachina," amesema.

Wang amesema timu hiyo itaweka kituo hicho cha watoto yatima kwenye ratiba yake ya kawaida ya kliniki ya kuhama kuhama, kupanga ziara za ufuatiliaji na kufanya ushirikiano na vituo vya afya vya huko katika utoaji huduma za afya ya mtoto, na kugeuza shughuli hiyo kuwa uungaji mkono endelevu.

Daktari akifanya upimaji kwa kutumia ultrasound kwenye shughuli ya huduma ya afya kwa umma iliyofanywa na Timu ya 36 ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania katika Kituo cha Watoto Yatima cha Kitumba, Kisiwa cha Unguja, Zanzibar, Tanzania, Novemba 21, 2026. (Timu ya 36 ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha