Kongamano lafanyika Ethiopia kuendeleza ushirikiano wa kitaaluma kati ya China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2026

Jeilu Oumer, Makamu Mkuu wa Taaluma wa Chuo Kikuu cha Addis Ababa, akitoa hotuba kwenye kongamano la kimataifa juu ya stadi za lugha na tamaduni za Aafrika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 24 Novemba, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Jeilu Oumer, Makamu Mkuu wa Taaluma wa Chuo Kikuu cha Addis Ababa, akitoa hotuba kwenye kongamano la kimataifa juu ya utafiti wa lugha na tamaduni za Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 24 Novemba, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

ADDIS ABABA - Kongamano la kimataifa juu ya utafiti wa lugha na tamaduni za Afrika limeanza jana Jumanne jijini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, likijikita katika kuendeleza ushirikiano wa kitaaluma, kuelewana kiutamaduni, na ubadilishanaji wa maarifa kati ya China na Afrika.

Kongamano hilo lenye kaulimbiu "Ubadilishanaji na Kufunzana kati ya Ustaarabu wa China na Afrika," limewakutanisha wasomi zaidi ya 100 wa lugha na utamaduni kutoka nchi 20 za Afrika na China.

Katika hotuba yake kuu kwenye kongamano hilo, Jeilu Oumer, Makamu Mkuu wa Taaluma wa Chuo Kikuu cha Addis Ababa, amesema kongamano hilo linatoa fursa muhimu ya kutafakari juu ya uhusiano wa muda mrefu kati ya China na Afrika, na kuimarisha zaidi ushirikiano wao wa kielimu, kitamaduni, na wa kimaarifa.

"Tunahamasishwa hasa na uhalisia kwamba lugha nyingi za Afrika sasa zinafundishwa na kusomwa katika Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU), jambo linalotengeneza fursa mpya za majadiliano na kuelewana kimaarifa. Mfano dhahiri ni kozi ya lugha na utamaduni wa Kiamhari (lugha rasmi nchini Ethiopia)," amesema Oumer.

Akisifu dhamira ya BFSU katika kuanzisha Shule ya utafiti wa Afrika, mahsusi kwa ajili ya kufanya utafiti wa historia, uchumi, jamii, utamaduni, na lugha za Afrika, Oumer amesema mafanikio hayo yanaonesha thamani ya ushirikiano uliojengwa katika kuheshimiana, mshikamano, na matarajio ya pamoja kwa ajili ya maendeleo.

Katika hotuba yake iliyorekodiwa, Zhao Gang, Makamu Mkuu wa BFSU, amesema kongamano hilo ni sehemu ya dhamira ya China na Afrika katika kujenga jumuiya ya hali zote ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.

"Mwaka huu, 2026, ni Mwaka wa Mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika. Ni mwaka muhimu sana wa kutekeleza maoni ya pamoja yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Viongozi wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na kuimarisha uhusiano kati ya watu wa China na Afrika," Zhao amesema.

Akibainisha kuwa Afrika na China zimeendeleza desturi za kimaarifa na urithi wa kitamaduni ulio tajiri na wa aina mbalimbali, Yekoyealem Desie, Mkuu Mtendaji wa Chuo cha Elimu na Utafiti wa Lugha katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, amesisitiza umuhimu wa kongamano hilo katika kutengeneza fursa, si tu kwa ajili ya kuelewana, bali pia kwa ajili ya kuzalisha maarifa mapya na kuimarisha uhusiano wa kati ya watu.

Washiriki katika kongamano hilo, lililoandaliwa kwa pamoja na Chuo cha Elimu na Utafiti wa Lugha cha Chuo Kikuu cha Addis Ababa na Chuo cha Utafiti wa Afrika cha BFSU, wamejadili kwa kina kuhusu lugha, mbinu za kufundisha, tafsiri, elimu ya kuvuka tamaduni, diplomasia, fasihi, uchapishaji, na utafiti wa kiisimu.

Yekoyealem Desie, Mkuu Mtendaji wa Chuo cha Elimu na Masomo ya Lugha katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, akitoa hotuba kwenye kongamano la kimataifa juu ya stadi za lugha na tamaduni za Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 24 Novemba, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Yekoyealem Desie, Mkuu Mtendaji wa Chuo cha Elimu na Utafiti wa Lugha katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, akitoa hotuba kwenye kongamano la kimataifa juu ya utafiti wa lugha na tamaduni za Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 24 Novemba, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Washiriki wakihudhuria kongamano la kimataifa juu ya stadi za lugha na tamaduni za Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 24 Novemba, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Washiriki wakihudhuria kongamano la kimataifa juu ya utafiti wa lugha na tamaduni za Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 24 Novemba, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha