人民网首页

Miundombinu

Zhangjiakou mkoani Hebei yafanya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imemalizika siku chache zilizopita, na viwanja vya vya michezo vya Yunding katika eneo la mashindano la Zhangjiakou mkoani Hebei vimeingia haraka kwenye kipindi cha maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi, ambayo itafanyika hivi karibuni. (Mpiga picha:Wu Diansen/Tovuti ya Picha ya Umma).

(Picha inatoka People's Daily Online.)

Wafanyakazi walinda kwa makini kwa pande zote usafirishaji salama wa treni za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

Reli ya Mwendokasi ya Beijing-Zhangjiakou inabeba jukumu la usafirishaji wa kuunganisha maeneo matatu ya mashindano ya michezo ya Beijing na Zhangjiakou, ili kuhakikisha huduma ya usafirishaji wakati wa siku za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Kila usiku wa manane , wafanyakazi wa treni za reli hiyo wanafanya upimaji kwa pande zote juu ya treni hizo, na kufanya jitihada zote kulinda usafiri salama wa treni kwa ajili ya mashindano ya michezo ya Olimpiki.

Maonesho ya Taa kwenye Mnara wa Olimpiki wa Beijing

Picha iliyopigwa Januari 29, 2022 ikionesha maonesho ya taa kwenye Mnara wa Olimpiki wa Beijing hapa Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Ding Xu).

(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Mnara wa Nembo ya Maduara Matano ya Olimpiki Wakaribisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

Hivi karibuni, kazi ya kufunga “Mnara wa Haituo” wa Nembo ya Maduara Matano ya Olimpiki imekamilika. Mnara huo uko kwenye eneo la michezo la Yanqing la Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na sasa ujenzi wa mradi huo umekaribia kukamilika.

1 2 3 4 Inayofuata