人民网首页

Miundombinu

Treni ya Michezo ya Olimpiki Yaonekana kwenye Kituo cha Chongli cha Reli ya Beijing-Zhangjiakou

Januari 6, Treni ya G9981 ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yakisimama kwenye Kituo cha Chongli cha Reli ya Beijing-Zhangjiakou. Habari zinasema, treni zote za michezo hiyo zitakuwa ni za mwendo kasi za Fuxing, ambazo kasi zao zinafikia kilomita 350 kwa saa, na ndani ya treni kuna studio za 5G.

Hii ni picha iliyopigwa Desemba 23 ikionesha Uwanja wa Kituo cha Kitaifa cha Michezo Miwili ya Majira ya Baridi katika Eneo la Michezo la Zhangjiakou. (Picha ilipigwa na UAV.)

Wiki ya Mazoezi ya Wanamicheo Katika Majira ya Baridi Yaanza

Kuanzia Tarehe 28 hadi Tarehe 31, Desemba, Kituo cha Kitaifa cha Michezo Miwili ya Majira ya Baridi kilichoko Eneo la Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi la Zhangjiakou, kitaanza wiki ya mazoezi ya wanamichezo wa nchi mbalimbali, ambayo ni shughuli ya mwisho katika mfululizo wa shughuli za majaribio za“Tukutane Beijing” za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Hivi sasa maandalizi mbalimbali ya uwanja huo yamekamilika.

Jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang likianza rasmi kutengeneza theluji. Mpiga picha: Li Qiang

Jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang laanza kutengeneza theluji

Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, alfajiri ya Jumatatu (leo), mashine nne za kutengeneza theluji, taa za usiku za jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji zimewashwa, hali ambayo inaonesha utoaji wa umeme kwenye uwanja huo wa michezo umefikia kigezo cha matumizi wakati wa mashindano, na jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang limeanza rasmi kutengeneza theluji. Jukwaa la kuteleza na kuruka juu ya theluji la Bustani ya Shougang liko ndani Bustani mpya ya Shougang katika Eneo la Shijinshan la Beijing.

Picha iliyopigwa Novemba 30, 2021, ikionesha mandhari mbalimbali za Bustani ya Shougang katika Wilaya ya Shijingshan, Beijing. (People's Daily Online/Peng Yukai)

Ndani ya Bustani ya Shougang: Utulivu kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

Bustani ya Shougang, ni eneo la kinu cha chuma lililogeuzwa kuwa Maeneo yenye shughuli za Kitamaduni na Michezo katika Wilaya ya Shijingshan Magharibi mwa Beijing. Kwa sasa imekuwa Makao Makuu ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kwa Walemavu ya Beijing Mwaka 2022.

Iliyopita1 2 3 4 Inayofuata