Rais Xi Jinping wa China amesema China na Ufaransa zina wajibu wa nchi kubwa wa kufanya jumuiya ya kimataifa kuwa na mshikamano ili kukabiliana na changamoto za kimataifa katika wakati ambao mabadiliko mengi mapya yanajitokeza katika mazingira ya kimataifa. Xi ameyasema hayo alipokutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika wakati wa kufanyika kwa Mkutano wa Viongozi wa G20 huko Rio de Janeiro, Brazil.
Rais Xi Jinping wa China amesema ushuru ulioongezeka wa Umoja wa Ulaya kwa magari ya umeme ya China unafuatiliwa duniani kote, ambapo China siku zote inasisitiza kutatua tofauti kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, huku ikitarajiwa kuwa Ujerumani itaendelea kufanya kazi yake muhimu katika suala hili. Rais Xi ameyasema hayo kwenye mkutano wake na Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani katika wakati wa kufanyika kwa Mkutano wa Viongozi wa G20 huko Rio de Janeiro, Brazil, akisistiza kuwa China inaiona Ulaya kama nguzo muhimu katika dunia yenye ncha nyingi, na kuongeza kuwa China imejitolea kushirikiana na Ulaya ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja na kukuza maendeleo endelevu na thabiti ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
Asubuhi ya Tarehe 19, Novemba kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China amewasili Brasilia kwa ziara ya kiserikali nchini Brazil. Baada ya kuwasili uwanja wa ndege alilakiwa na Rui Costa, mkurugenzi wa ofisi ya Ikulu ya rais pamoja na maofisa wengine waandamizi wa Brazil, ambapo wasanii wanawake wa Bendi ya Batala walipiga muziki wa ngoma ulio wa furaha na uchangamfu kwa kumkaribisha.