Rais Xi Jinping wa China Jumatatu alipotoa hotuba kwenye Mkutano wa 19 wa G20 kuhusu Mapambano Dhidi ya Njaa na Umaskini huko Rio de Janeiro, alielezea hatua nane za China kwa ajili ya maendeleo ya dunia. Hatua hizo ni pamoja na kufanya ushirikiano wa ujenzi wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja Njia Moja”.
Asubuhi ya Tarehe 18, Novemba kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China katika wakati wa kuhudhuria kwenye kipindi cha kwanza cha Mkutano wa 19 wa kundi la nchi 20 (G20) huko Rio de Janeiro, Brazil. (Picha na Li Xueren/Xinhua) Rais Xi Jinping wa China amesema China ingependa kushirikiana na pande zote ili kujenga dunia yenye maendeleo kwa pamoja, na ametoa hatua nane za China kwa ajili ya maendeleo ya dunia.
(Xinhua/Wang Tiancong) Kabla ya mkutano wa kilele wa G20 wa mwaka huu, wataalamu walisema kuwa, nchi za Afrika zinapaswa kutumia vizuri fursa ya kujiunga na kundi la nchi 20 (G20) ili kuhimiza biashara na uwekezaji na nchi zenye nguvu zaidi duniani. Sizo Nkala, mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Afrika na China ya Chuo Kikuu cha Johannesburg alipohojiwa na China Daily alisema kuwa, Umoja wa Afrika kujiunga na G20 ni hatua muhimu ya kuifanya Afrika iongeze zaidi kutambuliwa kwake kwenye jukwaa la kimataifa, na kutoa fursa kwa Afrika kujadiliana kwa usawa na nchi tajiri.