Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko mjini Rio de Janeiro kwa ziara ya kiserikali nchini Brazil na kuhudhuria Mkutano wa kilele wa 19 wa viongozi wa kundi la G20, amechapisha makala yenye kichwa cha "Urafiki Unaovuka Bahari Kubwa, Wakati Wafika Kufunga Safari Kuelekea Mustakabali wa Pamoja" jana Jumapili, tarehe 17 Novemba kwenye gazeti la Folha de S. Paulo la Brazil.
(Picha inatoka tovuti ya CRI) Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden siku ya Jumamosi kando ya Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC) mjini Lima, Peru. Rais Xi amesema kuwa uhusiano kati ya China na Marekani umepitia kipindi cha misukosuko, lakini chini ya uongozi wa pamoja wa marais hao wawili, pande hizo mbili pia zimekuwa zikifanya mazungumzo na ushirikiano wenye ufanisi na kwa ujumla uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kwa utulivu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema ombi la China kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa APEC mwaka 2026 limeungwa mkono na pande zote husika na kuidhinishwa katika mkutano wa viongozi wa APEC uliomalizika mwishoni mwa wiki. Akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu suala husika kwenye mkutano na waandishi wa habari, msemaji huyo ameeleza kuwa APEC ni mfumo muhimu wa ushirikiano wa kiuchumi katika eneo la Asia-Pasifiki na kwa kuzingatia hali ya jumla ya kukuza ushirikiano wa Asia-Pasifiki, China imejitolea kubeba majukumu yake na kutoa ombi la kuwa mwenyeji wa mkutano wa APEC wa 2026, ambalo limekaribishwa na nchi wanachama wa APEC na limeidhinishwa na mkutano wa viongozi wa APEC wa mwaka huu.
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Lima cha Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi) Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Lima cha Peru, Novemba 16, 2024.