Jumuiya ya Afrika Mashariki yakubali kufuata mpango wa kuwajengea vijana jukwaa la amani na usalama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2021

Jumatatu ya wiki hii, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilisema katika taarifa yake kuwa, ilipitisha mpango wa kuwajengea vijana jukwaa la kikanda la amani na usalama, ili kuwawezesha vijana washiriki zaidi katika mambo ya usalama ya Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo ilisema, baraza la EAC linatoa wito wa kuendeleza mfumo wa kuchora ramani ya maeneo yasiyo salama ambayo yanahitaji vijana kuingilia.

Katibu mkuu wa EAC Bw. Peter Mathuki alisema, mpango wa EAC wa miaka mitano ijayo ni kwa ajili ya kuimarisha usalama kwa kupitia kuweka mkazo katika kuendeleza sekta muhimu sana ya kibinafsi ili kuleta mali na nafasi za ajira.

"Mafanikio yatakayopatikana kwenye sekta hiyo yatapunguza ushawishi kwa vijana kushiriki kwenye shughuli za kuharibu usalama." Bw. Mathuki alisema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha