Tukio la mashambulizi latokea jijini Dar, watu wanne wauawa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 26, 2021

Tarehe 25, rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alisema kwamba, tukio la mashambulizi lilitokea jijini Dar es Salaam, Tanzania, tukio hilo limesababisha vifo vya polisi watatu na mlinzi mmoja wa kampuni ya ulinzi.

Rais Samia alisema kwenye mtandao wa kijamii kwamba, tukio la mashambulizi lilitokea mchana kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam, mshambuliaji mmoja alipiga risasi kuwaua polisi watatu na mlinzi mmoja, sasa hali imedhibitiwa. Rais Samia alitaka polisi kuchunguza tukio hilo, na alitoa salamu za rambirambi kwa waliouawa.

Msimamizi mkuu wa polisi ya Tanzania alipohojiwa na radio moja ya huko alisema, mshambuliaji alipigwa risasi na polisi akafa, polisi wanachunguza hali yake na kusudi lake.

Habari nyingine zilisema kwamba, tukio hilo lilitokea karibu na ofisi ya ubalozi wa Ufransa nchini Tanzania, licha ya kuuawa kwa watu wanne 4, wengine sita walijeruhiwa.

Muda mfupi kabla ya tukio hilo kutokea, rais Samia Suluhu Hassan alitoa hotuba akitaka polisi kuongeza nguvu ya kupambana na magenge ya uhalifu wa dawa za kulevya na vitendo vya ugaidi.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha