Syria yakubali gesi asilia na nishati ya umeme zisafirishwe kwa kupitia eneo lake kwa Lebanon

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2021

Tarehe 4, shirika la habari la Syria lilisema, kutokana na ombi la Lebanon, Syria imekubali gesi asilia iliyotoka Misri na nishati ya umeme iliyotoka Jordan zitasafirishwa kwa Lebanon kwa kupitia eneo la Syria, ili kusaidia kutatua tatizo la upungufu wa nishati ya Lebanon.

Ujumbe wa Lebanon uliwasili Syria tarehe 4, na ulifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Syria Bw. Mekdad na maofisa wengine wa nchi hiyo. Baada ya mazungumzo, katibu mkuu wa Kamati ya ngazi ya juu ya Syria-Lebanon Bw. Nasri Khoury alisema, pande hizo mbili zilijadili changamoto kubwa zinazozikabili nchi hizo mbili. Upande wa Lebanon unataka gesi asilia iliyotoka Misri na nishati ya umeme iliyotoka Jordan zitaweza kusafirishwa kwa kupitia eneo la Syria, "Syria ilikaribisha ombi hilo".

Hivi sasa Syria na Lebanon zote zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa nishati, na ombi husika la Lebanon yanalenga kupunguza hali hiyo mbaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha