Rais wa China Xi Jinping afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Kishida

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2021

Rais Xi Jinping wa China Ijumaa hii amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu mpya wa Japan Fumio Kishida.

 Akisisitiza kwamba China na Japan ni majirani wa karibu, Xi, akinukuu msemo wa kale wa China, alisisitiza kuwa ujirani mwema ni hazina ya nchi.

 Kudumisha na kukuza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Japan kunaendana na maslahi ya kimsingi ya nchi zote mbili na wananchi wake, na pia ni muhimu kwa amani na utulivu wa Asia na hata dunia nzima, ameongeza.

 Kwa sasa, uhusiano wa China na Japan unakabiliwa na fursa na changamoto kwa wakati mmoja, Xi alisema, akiongeza kuwa China inapongeza umuhimu ambao serikali mpya ya Japani inazingatia kudumisha mawasiliano ya hali ya juu kati ya nchi hizo mbili.

 Alisema, China iko tayari kushirikiana na Japani ili kuimarisha zaidi mazungumzo na ushirikiano, na kukuza ujenzi wa uhusiano wa China na Japan ambao unakidhi mahitaji ya enzi mpya yanayoichukua historia kama kioo na kufungua uhusiano wa siku zijazo.

 Kwa kuzingatia kwamba mwaka ujao China na Japan zitaadhimisha miaka 50 tangu kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati yao, China inatumai kuwa pande hizo mbili zitarejea tena matarajio yao ya msingi na kuendana kwa pamoja ili kutumia nafasi hii kufungua ukurasa mpya ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Xi alisema.

Xi alisema kwamba China na Japani zinapaswa kujifunza kwa makini kutoka kwa uzoefu chanya na hasi katika maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kufuata kwa uangalifu kanuni zilizowekwa katika nyaraka nne za kisiasa kati yao, na kutekeleza makubaliano ya kisiasa kuwa wao ni washirika na sio maadui.

Xi pia aliipongeza Japan kwa kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Tokyo na kuongeza kuwa China inaikaribisha Japan kushiriki kikamilifu kwenye Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi yatakayofanyika Beijing, China. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha