China yatumai Guinea kudumisha utulivu na maendeleo ya taifa: Msemaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2021

China inatumai pande zinazohusika nchini Guinea zitafanya juhudi kudumisha utulivu na maendeleo ya nchi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema Ijumaa iliyopita.

Zhao amesema hayo katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari alipoulizwa kutoa maoni juu ya mchakato wa kisiasa nchini Guinea.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Mamady Doumbouya, rais wa mpito wa Guinea, amemtaja Mohamed Beavogui kama waziri mkuu wa mpito wa taifa hilo.

Zhao alisema China inatumai kuwa pande husika nchini Guinea zitaendelea kufanya mazungumzo, na zitajitahidi kulinda utulivu na maendeleo ya taifa chini ya msaada wa mashirika ya kikanda na ya kimataifa.

Aliongeza kuwa China na Guinea zina urafiki wa muda mrefu, na China iko tayari kushirikiana na nchi hiyo kukuza maendeleo ya uhusiano na ushirikiano wa kirafiki kati yao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha