Picha: Bidhaa za utamaduni za COP15 zenye sura mpya zaongoza mtindo mpya wa kulinda mazingira (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2021
Picha: Bidhaa za utamaduni za COP15 zenye sura mpya zaongoza mtindo mpya wa kulinda mazingira
Kutokana na ongezeko la matumizi ya kahawa duniani, matatizo ya kushughulikia mabaki ya kahawa ya kiasi kikubwa yametokea. Kikombe hiki kilichotengenezwa kwa mabaki ya kahawa na raslimali mbadala salama na ngumu kinaweza kuoza kirahisi kwa asilimia 65. Na kifuniko chake kilitengenezwa kwa nyuzinyuzi za mwanzi, kwa hivyo ni chepesi sana. (Tovuti ya Gazeti la Umma/Weng Qiyu)

Boksi jepesi la kuwekea chakula na kikombe cha kahawa vilivyotengenezwa kwa mabaki ya kahawa, “penseli ya daima” isiyotumia wino, rangi ya midomo inayotengenezwa kwa mimea……Katika ukumbi wa Mkutano wa 15 wa pande zilizosaini “Mkataba wa Anuwai ya Viumbe” (COP15) uliofanyika huko Kunming, mkoa wa Yunnan, bidhaa hizo za utamadani zenye sura mpya zilizotengenezwa kwa raslimali mbadala zisizo na uchafuzi kwa mazingira zimevutia watazamaji wengi.

 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha