China yatoa mwito wa kusimamisha mapigano nchini Yemen, kuboresha hali ya kibinadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2021

UMOJA WA MATAIFA - Mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa (UN) Alhamisi wiki hii ametoa mwito wa kusimamisha mara moja mapigano nchini Yemen na kufanya juhudi ili kuboresha hali ya kibinadamu nchini humo.

Naibu Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Geng Shuang amesema, uhasama umezidi hivi karibuni nchini Yemen. China ina wasiwasi mkubwa juu ya hali hii na inahimiza pande zote kusimamisha mapigano mara moja na kumaliza vurugu, hasa kusimamisha mapigano huko Marib mapema iwezekanavyo. ,.

China inalaani mashambulio yote dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia, na inahimiza pande zote kufuata sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kulinda watu walioko hatarini, hususani wanawake na watoto, amesema katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tarehe 28 Septemba, Waziri Mkuu wa Yemen Maeen Abdulmalik Saeed na maafisa wengine wakuu walirudi Aden. China inakaribisha maendeleo hayo na inaunga mkono utawala wa serikali ya Yemen huko Aden. Pande zote zinazohusika zinapaswa kutekeleza makubaliano ya Riyadh, kudumisha usalama na utulivu huko Aden, na kutoa mazingira mazuri kwa serikali kuchukua hatua za kuboresha uchumi na maisha ya watu, amesema.

Geng Shuang amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Hans Grundberg amefanya juhudi kuwasilisha pande zote nchini Yemen na ametembelea nchi mbalimbali za kanda hiyo, China inapongeza juhudi zake. "Tunamhimiza mjumbe huyo maalum kuendelea na majadiliano ya kina na pande zinazohusika na mgogoro wa Yemen ili kuendeleza mazungumzo kati ya serikali ya Yemen na Kundi la Wahouth, na kutoa mpango wa kurejesha usalama nchini Yemen kwa wakati mwafaka.”

Amesema, azimio la suala la Yemeni haliwezi kupitishwa bila uratibu na ushirikiano wa nchi za kanda hiyo. Kurejesha amani na utulivu nchini Yemen ni maslahi ya pamoja ya nchi za kanda hiyo. China inazitaka pande zote zilizo na ushawishi nchini Yemen kuongeza juhudi zao za kutimiza amani na kuchukua hatua zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha