Mkutano wa 6 wa Vijana wa China na Afrika wafanyika Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2021
Mkutano wa 6 wa Vijana wa China na Afrika wafanyika Beijing
(Picha zinatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Asubuhi ya tarehe 19, Oktoba, Mkutano wa 6 wa vijana wa China na Afrika ulifanyika kwenye Kituo cha mawasiliano ya teknolojia na utamaduni ya vijana cha Song Chingling cha China hapa Beijing. Mkutano huo uliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje, na kuendeshwa na mfuko wa Song Chingling wa China, na uliwaalika wanafunzi wa Afrika wanaosoma Beijing na wajumbe wa vijana 45 kutoka nchi 44 za Afrika kuhudhuria kwenye mkutano.

Siku hiyo, vijana hao walishiriki kwenye shughuli mbalimbali za utamaduni wa jadi wa China katika kituo hicho, ambapo walijaribu uigizaji wa Opera ya Kibeijing, matibabu ya jadi ya China, muziki wa jadi, utarizi, kuchapa na kupiga rangi kwenye kitambaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha