Chuo Kikuu cha Addis Ababa cha Ethiopia kuanza kutoa Shahada ya Kwanza ya Lugha ya Kichina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2021
Chuo Kikuu cha Addis Ababa cha Ethiopia kuanza kutoa Shahada ya Kwanza ya Lugha ya Kichina
Picha 1: Mwanafunzi akiingia katika jengo la ofisi katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa huko Addis Ababa, Ethiopia, Oktoba 14, 2021. Chuo Kikuu cha Addis Ababa cha Ethiopia (AAU) kimetangaza kuwa kimekamilisha maandalizi ya kuzindua programu ya kwanza ya masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sanaa (MA) ya Lugha ya Kichina nchini Ethiopia (Xinhua / Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Chuo Kikuu cha Addis Ababa cha Ethiopia (AAU) kimetangaza kuwa kimekamilisha maandalizi ya kuzindua programu yake ya kwanza ya masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sanaa (MA) katika lugha ya Kichina nchini Ethiopia.

Shahada hiyo ya Pili ya kufundisha lugha ya Kichina kwa watu wanaoongea lugha nyingine (MTCSOL) ambayo ni ya kwanza katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, itatolewa na Chuo cha AAU kwa msaada wa Taasisi ya Confucius katika chuo hicho.

Emebet Mulugeta, Naibu mkuu wa Taaluma wa AAU, amesema kuwa kuanzisha kwa programu hiyo ya MTCSOL kutaketa nguvu inayohitajika katika kueneza lugha ya Kichina nchini Ethiopia na kukuza uhusiano kati ya watu katika nchi hizo mbili.

"Tulithamini sana na kuunga mkono mpango huu, na ilikuwa katika kipindi kifupi sana ambacho tathmini imefanywa na kupitishwa na baraza la seneti, ambalo ndilo chombo cha juu zaidi cha kutoa maamuzi cha chuo kikuu," Mulugeta ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

 "Idara ya lugha ya Kichina ya chuo chetu imekuwa ikitoa Shahada ya Kwanza ya Sanaa (BA) kwa muda mrefu, na wahitimu hao wanahitaji kuwa na uwezo zaidi na ujuzi zaidi katika lugha hiyo. Ni muhimu kuanzisha programu hii ya shahada ya uzamili ili tuweze kuboresha wale wanafunzi ambao tayari wamemaliza shahada ya kwanza” amesema.

Aidha, Mulugeta amesema kuwa, Chuo Kikuu cha AAU na Taasisi ya Confucius katika chuo hicho zinapaswa kufanya juhudi za pamoja ili kuleta matokeo yanayotarajiwa katika programu hiyo.

Takwimu kutoka taasisi hiyo inaonyesha kuwa, taasisi ya Confucius ya AAU, ambayo ilianza kufanya kazi nchini Ethiopia Mwaka 2012, hadi sasa imedahili zaidi ya wanafunzi 10,000 waliofaulu katika viwango tofauti vya masomo ya lugha ya Kichina. Zaidi ya wahitimu 100 wameweza kupata Shahada zao za Kwanza za Lugha ya Kichina.

"Taasisi ya Confucius ni moja ya taasisi yenye uhai katika chuo chetu. Namna wanavyofundisha wanafunzi, uhusiano wao na wanafunzi, na soko la ajira kwa wanafunzi ni sababu nyingine kuu ambazo zilitulazimu kuanzisha programu hii ya masomo” Amenuael Alemayehu, Mkuu wa Kitivo cha Masomo ya Binadamu, Lugha, Uandishi wa Habari na Mawasiliano ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Confucius katika AAU, programu ya MTCSOL ya miaka miwili kwa muda wote, ambapo katika mwaka wa kwanza wanafunzi watasoma kozi za msingi zilizopangwa katika Chuo cha AAU na wanafunzi watakaokufaulu wataendelea na masomo ya ufundishaji wa lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Teknolojia na Elimu cha Tianjin nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha