Watu wa Afrika wasema Chanjo kutoka China ni kama “mvua kwa wakati”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2021

Kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Dakar, Senegal, Novemba 29, China iliahidi kwa dhati kuwa itatoa tena dozi bilioni 1 za chanjo dhidi ya korona kwa Afrika. Baadhi ya Waafrika kutoka nyanja mbalimbali waliofanyiwa mahojiano wanaamini kwamba, chanjo hizo zilizoahidiwa na China ni kama “mvua kwa wakati”, kwani ni muhimu sana katika mapambano dhidi ya janga la koronana kuzuia kuenea kwa virusi vya korona.

Mtaalam wa masuala ya kimataifa wa Kenya Cavins Adhill alisema Tarehe 29 Novemba kwamba, kwa sasa idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa korona imeongezeka kwa sababu ya kuathiriwa na virusi vipya vya korona aina ya Omicron, hivyo, kitendo cha China kuahidi kutoa chanjo kwa Afrika ni kama “mvua inayonyesha kwa wakati”, kinaonesha uungaji mkono wa dhati wa China kwa Afrika tangu janga la korona lilipuke.

Nchini Zimbabwe, kutokana na maendeleo mazuri ya udungaji wa chanjo na maofisa wakuu wa serikali kuonesha mifano, watu wengi zaidi wametambua umuhimu wa kudungwa chanjo na usalama na umakini wa chanjo kutoka China, na wamejiunga na zoezi la udungaji wa chanjo. Wamesifu ushirikiano kati ya China na Zimbabwe katika chanjo kwa maisha na afya ya Raia wa Zimbabwe na kusema kuwa wanaamini sana chanjo kutoka China.

Francis Litupi ni muuzaji wa magazeti kwenye kibanda kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Alichagua kudungwa chanjo kutoka China kwa kuwa aliamini katika usalama wa chanjo hizo. Katika mahojiano na mwandishi wa habari, alisema, hatua ya China kuahidi kutoa tena dozi bilioni 1 za chanjo dhidi ya korona kwa Afrika inaonesha Afrika na China ni marafiki wanaoshirikiana katika kukabiliana na taabu kwa pamoja, “Chini ya uungaji mkono wa China, Afrika itaweza kudhibiti janga la korona.”

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha