Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China wafungwa

(CRI Online) Machi 10, 2022
Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China wafungwa
Kikao cha ufungaji cha Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) kikifanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2022. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China umefungwa leo baada ya kumaliza ajenda mbalimbali kwa mafanikio.

Viongozi wa Chama na serikali akiwemo rais Xi Jinping wamehudhuria ufungaji wa mkutano huo.

Mkutano huo umepitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya Baraza hilo, azimio kuhusu utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa tokea Mkutano wa 4 wa Baraza hilo, ripoti kuhusu uthibitishaji wa mapendekezo mapya , na azimio la kisiasa la mkutano huo.

 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha