Puto linaloelea angani lililoundwa na China lavunja rekodi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2022
Puto linaloelea angani lililoundwa na China lavunja rekodi
Puto linaloelea angani "Jimu No.1" aina ya III likijazwa upepo katika Tarafa ya Zhaxizom ya Eneo la Tingri, katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, nchini China Mei 12, 2022. Meli hiyo ya Puto la kuelea angani lililoundwa nchini China kwa ajili ya ufuatiliaji wa hali ya hewa angani, liliruka angani na kuelea kwa urefu uliovunja rekodi wa Mita 9,032 jana Jumapili. Meli hiyo ya "Jimu No.1" aina ya III iliyoundwa na Idara ya Utafiti wa Upashanaji wa Habari za Usafiri wa Anga ya Taasisi ya taifa ya Sayansi ya China (CAS) ina ujazo wa mita za ujazo 9,060. (Xinhua/Jiang Fan)

LHASA - Puto linaloelea angani, ambalo liliundwa nchini China kwa ajili ya uchunguzi wa hali ya hewa angani, limepaa na kuelea angani kwa umbali uliovunja rekodi Mita 9,032 katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet ya China siku ya Jumapili.

Ikiwa limeundwa na Idara ya Utafiti wa Upashanaji wa Habari za Usafiri wa Anga ya Taasisi ya Taifa ya Sayansi ya China (CAS), Puto hilo la "Jimu No.1" aina ya III lina ujazo wa mita za ujazo 9,060.

Puto hilo linaweza kukusanya data katika mwinuko wa juu, ambazo hutumiwa kufuatilia mzunguko wa maji wa eneo husika na kufuatilia mabadiliko katika muundo wa hewa kwenye anga.

Mradi huo, ambao ni sehemu ya utafiti na uchunguzi wa pili wa kisayansi wa China katika eneo la Uwanda wa Qinghai-Tibet, unatekelezwa na wanasayansi 64 kutoka taasisi kadhaa za utafiti za China.

“Puto hilo la kuelea angani pia litatoa data muhimu juu ya chanzo cha maji cha Miiunuko ya juu ya Qinghai-Tibet, na kuchangia katika kukabiliana na athari za maji, ikolojia na shughuli za binadamu chini ya mabadiliko ya tabianchi” , anasema Yao Tandong, mtafiti katika CAS na kiongozi wa timu ya pili ya utafiti wa kisayansi katika eneo la Mililma ya Qinghai-Tibet.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha