

Lugha Nyingine
Hospitali yafunguliwa karibu na mlango wa nyumbani
![]() |
Daktari wa Kituo cha Huduma ya Afya cha Makazi ya Lugouqiao akifanya matibabu kwa wakazi katika Makazi ya Zhujiangzitai ya Mtaa wa Qingta wa Eneo la Fengtai la Beijing. (Picha ilipigwa Mei 22.) |
Kutokana na athari ya maambukizi ya virusi vya korona, kuanzia saa 6 ya Tarehe 17, Mji wa Beijing ulichukua hatua ya usimamizi na udhibiti wa muda kwa Mitaa ya Qingta, Wulidian na Lugouqiao na mingineyo.
Mitaa, makazi na vituo vya huduma ya afya vya makazi zilichukua hatua mbalimbali pamoja ili kukidhi mahitaji ya matibabu na dawa za wakazi walioko kwenye maeneo yanayofanyiwa usimamizi na udhibiti wa muda.
Kituo cha Huduma ya Afya cha Makazi ya Lugouqiao kiliunda “timu maalum ya matibabu kwa maeneo ya usimamizi na udhibiti”, kikikidhi mahitaji ya matibabu ya wakazi kwa njia za kujiandikisha na madaktari wa kifamilia na wahudumu maalum wa matibabu, kufungua kituo cha matibabu katika maeneo ya udhibiti, kutoa huduma za kuandikisha dawa na kupeleka nyumbani na au kuagiza matibabu ya nyumbani.
(Mpiga picha: Peng Ziyang/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma