Habari picha: Msanii achora michoro ya kuvutia kwenye kuta huko Yongsheng nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2022
Habari picha: Msanii achora michoro ya kuvutia kwenye kuta huko Yongsheng nchini China
Liu Zhicheng (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanakijiji baada ya kumaliza kuchora ukutani katika Wilaya ya Yongsheng, Mji wa Lijiang, Mkoa wa Yunnan nchini China, Juni 24, 2022. Mchoraji wa michoro ya ukutani bila faida wa "baada ya miaka ya 95", anayetoka Wilaya ya Yongsheng, Mji wa Lijiang, amejipatia umaarufu miongoni mwa wanakijiji katika eneo amalotoka na watu kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.
Msanii huyo aitwaye Liu Zhicheng amechora zaidi ya michoro 20 ya ukutani yenye mandhari tofauti katika vijiji vingi vya kwenye eneo alikozaliwa. Kazi zake za sanaa zimeongeza rangi kwenye vijiji na kuvutia watalii wengi kufuatia kutengeneza video fupi zilizorekodi mchakato wa uchoraji kuanza kuenezwa kwenye mtandao. "Ni heshima yangu na furaha yangu kuwa na nafasi ya kuboresha mazingira kwa kutumia usanii wangu," Liu amesema. (Xinhua/Jiang Wenyao)
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha