

Lugha Nyingine
Mji wa Shanghai nchini China watangaza tahadhari nyekundu kutokana na halijoto ya juu
SHANGHAI - Idara ya uchunguzi wa hali ya hewa ya Mji wa Shanghai nchini China imetoa tahadhari nyekundu ya joto kali siku ya Jumapili huku halijoto katika baadhi ya maeneo ya mji huo ikipanda hadi nyuzi joto 40.
Shanghai imeshuhudia halijoto ya juu kwa siku sita mfululizo kuanzia Julai 5. Halijoto katika Kituo cha Xujiahui Shanghai ilifikia nyuzi joto 40 saa 8 na dakika12 mchana ya Jumapili, ikiwa joto la juu zaidi ya nyuzi joto 40 tangu Shanghai ilipoanzisha kurekodi hali ya hewa Mwaka 1873.
Jumla ya siku 15 zenye joto kali zaidi ya nyuzi joto 40 zimeripotiwa katika mji huo tangu 1873, na nyuzijoto 40.9 Mwaka 2017 ziliweka rekodi.
Kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa wa hivi punde, Shanghai itaendelea kushuhudia hali ya hewa ya joto la juu wiki ijayo kwa sababu hali ya hewa ya joto ya tropiki ndogo kuwa juu.
Idara ya hali ya hewa ya mji huo imeshauri umma kuepuka shughuli za nje majira ya saa sita mchana. Wakati wa kukutana na kizunguzungu, jasho kubwa, au udhaifu wa kiungo, watu wanashauriwa kwenda mahali penye hewa na kunywa maji ya chumvi ili kuzuia kiharusi cha joto.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma