Kituo cha Uzalishaji wa Umeme kwa nishati ya jua kinachojengwa kwa msaada wa China chapunguza uhaba wa umeme wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2022
Kituo cha Uzalishaji wa Umeme kwa nishati ya jua kinachojengwa kwa msaada wa China chapunguza uhaba wa umeme wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Picha iliyopigwa Juni 2 ikionesha Kituo cha Uzalishaji wa Umeme kwa nishati ya jua cha Sakai kilichoko katika Mji wa Bimbo, Jamhuri ya Afrika ya Kati.(picha na droni)

Kituo cha Uzalishaji wa Umeme kwa nishati ya jua cha Sakai kiko katika Mji wa Bimbo, kilomita 9 hivi magharibi mwa Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, kilijengwa kwa msaada wa Kampuni ya Ujenzi wa Umeme ya Tianjin ya Kundi la Ujenzi wa nishati la China, na jumla ya uwezo wa uzalishaji ni kilowatisaa elfu 15, kuzinduliwa kwake kumepunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa umeme huko Bangui na kuhimiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya huko.

Katika muda mrefu uliopita, tatizo la uhaba wa umeme lilisumbua watu wa eneo hilo: kukatika kwa umme ni hali ya kawaida, hata umeme uliweza kukatika kwa wiki mbili au tatu; baada ya machweo, ni vigumu kwa watoto kusoma, na mitaani humo kulikuwa giza totoro, hakuna mtu aliyethubutu kwenda nje.

Katika kipindi cha Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Septemba, 2018, China na Jamhuri ya Afrika ya Kati zilifikia makubaliano kuhusu ujenzi wa mradi huo. Aprili, 2021, wajenzi wa Kampuni ya Ujenzi wa Mradi wa Umeme ya Tianjin walikwenda Jamuhuri ya Afrika ya Kati kufanya ujenzi. Kituo hicho kilianza kufanya kazi Juni 15 mwaka huu. Habari zilisema kuwa kituo hicho cha uzalishaji wa umeme sasa kinaweza kukidhi 30% ya mahitaji ya umeme mjini Bangui.

Yangdu Anji, mkazi wa Mji wa Bangui, aliwaambia waandishi wa habari kuwa baada ya kuwa na kituo hicho, jokofu inaweza kutumika, na tunaweza kupata maji ya barafu siku za joto; watoto wangu wanaweza kusoma wakati wa usiku, na sasa ninatumai wanaweza kupata alama nzuri."

Nanbama, mkazi anayeishi katika kitongoji cha Mji wa Bangui, alisema kuwa sasa kuna taa nyingi nje wakati wa usiku, na wakazi wanaona usalama zaidi.

Zhang Zhiguo, meneja wa mradi wa kituo hicho alifahamisha kuwa, hivi sasa Bangui inategemea zaidi mafuta ya dizeli na nishati ya maji katika kuzalisha umeme. Gharama ya mafuta ya dizeli ni kubwa na hali ya maendeleo ya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji ni ya polepole. Na ujenzi wa kituo hicho ulifanyika kwa muda mfupi zaidi, uzalishaji wake wa umeme ni bila kuleta uchafuzi kwa mazingira, na uwezo wake ni mkubwa, ambao umetatua kwa haraka tatizo la uhaba wa umeme wa huko. Wakati wa mchakato wa ujenzi, mradi huo ulitoa nafasi za ajira kwa watu wapatao 700 na kusaidia wafanyikazi wa huko kupata ufundi mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha