Mji mdogo wenye maumbo ya unajimu katika Mkoa wa Guizhou nchini China
 |
Watu wakitembelea jumba lenye umbo la sayari kwenye Kitongoji cha Kedu katika Eneo la Pingtang, Mkoa wa Guizhou nchini China, Julai 20, 2022. Mwaka 2007, Eneo la Pingtang lilizindua mpango wa kuhamisha watu uliohusisha wakazi 6,653 wa vijijini kutoka vitongoji vya Kedu na Tangbian. Mpango huo ulitekelezwa ili kuandaa mazingira ya ujenzi wa FAST (Redio ya Lenzi ya Mduara ya Darubini ya Redio yenye urefu wa Mita mia tano), inayojulikana pia kama "Jicho la China la Anga."
Mji mdogo wa Kedu ulianza mpango wa kujigeuza kuwa mji wenye maumbo ya unajimu kuanzia Septemba 2015, ukitumia fursa ya ukaribu wake na FAST. Kedu sasa ina zaidi ya miradi 20 iliyojengwa ili kuhimiza sayansi ya anga. Wakazi wengi wa vijijini waliohamishwa wamepata kazi au kuanzisha biashara zao katika eneo hilo. (Xinhua/Ou Dongqu) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)