Shanghai yafungua kituo cha mapumziko kwa wafanyakazi wanaofanya kazi nje katika majira ya joto (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2022
Shanghai yafungua kituo cha mapumziko kwa wafanyakazi wanaofanya kazi nje katika majira ya joto
Katika mkusanyiko huu wa picha zilizopigwa tarehe 16, Agosti, picha ya kushoto ikionesha mhudumu wa usafishaji mtaani Yang Xiucong akisafisha barabara; picha ya kulia ikionesha Yang akitumia simu kwenye kituo cha mapumziko cha eneo la Hongkou la Shanghai, China.

Hali joto ya hewa ya mwaka huu imeleta changamoto kubwa kwa wafanyakazi wanaofanya kazi nje ya nyumba huko Shanghai. Hivi karibuni, kituo kilichofunguliwa kwenye Mtaa wa Sanhe wa eneo la Hongkou la Shanghai kimewasaidia wahudumu wa usafishaji mtaani, wafanyakazi wa bustani, wa ujenzi wa mji na kazi nyingine mbalimbali wanaofanya kazi karibu nacho kupata mapumziko ya kuepuka hali joto ya hewa. (Xinhua/Liu Ying)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha