Wahudumu wa kutoa tahadhari juu ya mawimbi makali kando za Mto Qiantangjiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 13, 2022
Wahudumu wa kutoa tahadhari juu ya mawimbi makali kando za Mto Qiantangjiang
Septemba 12, wahudumu wa Timu ya kutoa tahadhari juu ya mawimbi makali ya mto Fu Banghua, Jia Wenjun na Gao Shaofeng wakiangalia kwa makini katika sehemu moja ya kingo ya Mto Qiantangjiang, ambapo kila mara kuna watu waliokaa huko kuvua samaki.

Siku za kabla na baada ya tarehe 15 ya Mwezi wa 8 kwa kalenda ya kilimo ya China, yaani sikukuu ya mbalamwezi ya jadi ya China ni wakati wa kufaa zaidi kwa kutazama mawimbi makubwa ya Mto Qiantangjiang yanayoshangaza na kufurahisha watu, na pia ni wakati wa pilikapilika kwa wahudumu wa kutoa tahadhari.

Katika siku za hivi karibuni, ili kuhakikisha usalama wa watu na watalii wanaotazama mawimbi ya mto, wahudumu Gao Shaofeng, Fu Banghua na Jia Wenjun wa Mtaa wa Xinjie wa Eneo la Xiaoshan la Mji wa Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang walifanya doria kwenye kingo cha mto. Kazi yao ni kulinda usalama wa sehemu moja ya Mto Qiantangjiang yenye urefu wa kilomita 1.9. Kila siku, wanafanya kazi ya kutoa tahadhari na kuwataka watazamaji waondoke kutoka sehemu yenye hatari, kuwashawishi watu waliovua samaki waondoke , na kukagua hali ya majengo ya ulinzi kwenye kando za mto huo, hivyo wanaitwa kuwa wahudumu wa kutoa tahadhari juu ya mawimbi makali. Hivi sasa, kuna wahudumu 372 katika kando mbili za Mto Qiantangjiang.

(Mpiga Picha: Jiang Han/xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha