

Lugha Nyingine
Picha kubwa za kale zilizochongwa kwenye kuta za mawe zagunduliwa katikati mwa China (5)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2022
Watafiti wa mabaki ya kale Jumatano ya wiki hii walisema, picha mbili kubwa zilizochongwa kwenye kuta katika wakati wa Enzi ya Song (B.K.960-1127) zimefukuliwa katika Mkoa wa Henan, katikati mwa China. Hizi ni picha kubwa zaidi zilizochongwa kwenye kuta kati ya picha kama hizo zilizogunduliwa nchini China.
Picha hizi za kuta zilifukuliwa kwenye magofu ya Zhouqiao ya Mji wa Kaifeng, Henan, kuta hizo zinagawanyika kwa kulingana kwenye kando mbili za upande wa Mashariki wa Daraja la Zhouqiao.
Picha zilizochongwa kwenye kuta zina kimo cha mita 3.3. Urefu wa sehemu yake kwenye kando ya kusini iliyogunduliwa ni mita 23.2 na urefu wa sehemu yake kwenye kando ya kaskazini iliyogunduliwa ni mita 21.2.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma