Picha kubwa za kale zilizochongwa kwenye kuta za mawe zagunduliwa katikati mwa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2022
Picha kubwa za kale zilizochongwa kwenye kuta za mawe zagunduliwa katikati mwa China
Picha iliyopigwa tarehe 21, Septemba, 2022 ikionesha michoro iliyochongwa kwenye kuta ambayo ni yenye alama ya jadi ya baraka katika utamaduni wa China iliyogunduliwa kwenye magofu ya daraja la Zhouqiao la Mji wa Kaifeng, Mkoa wa Henan wa katikati mwa China. (Xinhua/Li An)

Watafiti wa mabaki ya kale Jumatano ya wiki hii walisema, picha mbili kubwa zilizochongwa kwenye kuta katika wakati wa Enzi ya Song (B.K.960-1127) zimefukuliwa katika Mkoa wa Henan, katikati mwa China. Hizi ni picha kubwa zaidi zilizochongwa kwenye kuta kati ya picha kama hizo zilizogunduliwa nchini China.

Picha hizi za kuta zilifukuliwa kwenye magofu ya Zhouqiao ya Mji wa Kaifeng, Henan, kuta hizo zinagawanyika kwa kulingana kwenye kando mbili za upande wa Mashariki wa Daraja la Zhouqiao.

Picha zilizochongwa kwenye kuta zina kimo cha mita 3.3. Urefu wa sehemu yake kwenye kando ya kusini iliyogunduliwa ni mita 23.2 na urefu wa sehemu yake kwenye kando ya kaskazini iliyogunduliwa ni mita 21.2. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha