Hospitali iliyojengwa na China nchini Kuwait yafanyiwa hafla ya ufunguzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 21, 2022
Hospitali iliyojengwa na China nchini Kuwait yafanyiwa hafla ya ufunguzi
Picha hii iliyopigwa Tarehe 18 Desemba 2022 ikionyesha jengo kuu la Hospitali ya Uhakikisho wa Afya ya Kuwait huko Ahmadi, Kuwait. Hafla ya ufunguzi wa hospitali iliyojengwa na kampuni ya China imefanyika Ahmadi, Kuwait, Jumapili. (Picha na Asad/Xinhua)

Mradi wa Hospitali za Uhakikisho wa Afya wa Kuwait uliojengwa na Kampuni ya Metallurgiska ya China utatoa huduma za bima ya matibabu kwa wageni pekee. Inajumuisha hospitali mbili za Ahmadi na Al Jahra, zenye eneo la ujenzi la mita za mraba 85,000 na thamani ya kandarasi ya karibu dola milioni 500 za Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha